BREAKING NEWS
Showing posts with label Alikiba. Show all posts
Showing posts with label Alikiba. Show all posts

Monday, 18 July 2016

Download & Listen | Nyimbo Zote Za Alikiba Hapa

Saturday, 2 July 2016

Alikiba Atambua Kiu ya Mashabiki Zake, Asema Haya

Alikiba amesema anaamini mashabiki zake mpaka sasa watakuwa na kiu ya kusikiliza kazi mpya kutoka kwake hivyo hata waangusha kwani kwa sasa yeye atakuwa akitoka kazi juu ya kazi ili aende sawa na mashabiki zake.

“Ukiwa kama shabiki yangu number moja click link kwenye Bio yangu kufikisha 2 Million Views. Kisha baada ya hapo wewe shabiki yangu una haki ya kunidai mashine nyingine. Najua fika una kiu ya kusikia nini nimekuandalia. Asikwambie mtu ni mkwaju juu ya mkwaju. Twende sawa ila tusisahau ibada.” alisisitiza Alikiba

Friday, 1 July 2016

Diamond Platnumz Aweka Picha Ya Alikiba Kwenye Ofisi Yake, Itazame Hapa...!

Meneja wa Diamond, Babu Tale ameonyesha kuwa wao hawana tatizo na Alikiba baada ya kupost kipande cha video kinachoonyesha picha ya msanii huyo ndani ya studio ya Wasafi Records.
Bongo
Ni muda mrefu imezungumzwa kuwa Diamond na Alikiba wana bifu mpaka kupelekea kuanzishwa kwa baadhi ya team za mitandaoni za kukejeli mafanikio ya msanii wa team nyingine lakini hiyo ni dalili kuwa ipo siku itabaki historia tu.
Babu Tale alipost kipande hicho cha video kinachoonyesha baadhi ya picha za wasanii wakubwa Bongo akiwemo Marehemu Bi Kidude, Mr Blue, Dully Sykes, Juma Nature, Q Chief, Alikiba na wengine wengi.
Je, hiyo inaweza ikawa ndiyo kiki ya kuikaribisha video ya wimbo mpya wa Diamond aliowashirikisha P Square ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni?
Tazama video hapa.

Sunday, 12 June 2016

Download New Video | Nuh Mziwanda Ft. AliKiba - Jike Shupa


WATCH VIDEO
                                                                                       DOWNLOAD MP4


OR TEST BELOW


FOR MOBILE VIDEO

Wednesday, 8 June 2016

Download New Audio | Mr Blue ft Alikiba - Mboga Saba

                                 Audio |  Mr Blue ft Alikiba - Mboga Saba| Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/99156

  

Sunday, 5 June 2016

Ali Kiba Akubali Kua ni Kweli Hajui Kingereza

Ni mara chache sana unakutana na msanii na anakubali kua lugha ya kiingereza inampiga chenga. Nakumbuka msanii AY alikubali kua miaka kama 13 nyuma hakua akiiongea kugha hiyo kwa ufasaha lakini baada ya mazoezi mengi kwa sasa yupo vizuri.

Siku chache zilizopita msanii Ali Kiba alikubali kua pamoja na kukaa katika gemu mda mrefu na kukutana na wasanii wengi wa nje lugha hiyo bado ni tatizo kwake. Japo anaweza kuongea kidogo sana kwa Kingereza ila si mtaalamu sana. Msikie hapa akifunguka kuhusiana na swala hilo....

Monday, 30 May 2016

Alikiba Akanusha Kumuimbia Jokate Wimbo ‘Aje’

Alikiba amesema Aje si wimbo aliomuimbia Jokate wala msichana yeyote bali aliimba kwaajili ya mashabiki wake.
jo-e1434705782158
“Sijamuimbia mtu yeyote kwa kweli, mi nimeimba kwa ajili ya mashabiki wangu, kwanza sijawahi kumuimbia mtu kabisa, sijawahi, so ni kwa ajili ya mashabiki wangu,” Kiba alikiambia kipindi cha Friday Night Live cha EATV.
Hata hivyo Kiba alikiri kuwa kumtaja Wema kwenye wimbo huo kimekuwa ni kitu cha surprise kwa mrembo huyo.
Aje ni miongoni mwa nyimbo zinazofanya vizuri kwa sasa si tu Tanzania, bali sehemu nyingi za Afrika.

Meneja wa Alikiba Afanunua Nini Kitakachokuwepo Kwenye Alikiba TV

Series ya taarifa kubwa za michongo ya kimataifa aliyopata Alikiba mwezi huu imeendelea.

Wikiendi iliyomalizika, kampuni ya usimamizi inayofanya kazi naye, Rockstar4000 imetangaza kuingia naye ubia kwa kuanzisha kile kilichopewa jina ‘Alikiba TV.’

Kwa wengi taarifa hiyo iliyoandikwa kwa Kiingereza haijaeleweka vizuri na hivyo nimelazimika kumtafuta meneja wake, Seven Mosha kumuomba atupe ufafanuzi zaidi.

“Aikiba amezindua Alikiba TV ambayo ni content kuhusiana na kazi yake – matukio yote around him kikazi itakayokuwa inapatikana kwenye YouTube channel yake na pia itaanza kuoneshwa kwenye vituo mbalimbali tukianza na SoundCity,” Seven ameiambia Bongo5.

“Alikiba TV itakuwa chini ya mwavuli wa Rockstar Television,” ameongeza.

Kwa mujibu wa tangazo hilo zaidi ya Soundcity ya Nigeria, vituo vingine vya runinga duniani vitakavyoshirikiana naye kwenye mradi huo vitatangazwa. Kwa sasa mashabiki wameombwa kusubcribe kwenye channel yake ya Youtube ili kutopitwa na chochote.

Wiki mbili zilizopita Alikiba alisainishwa recording deal na label maarufu duniani, Sony Music. Kiba anayefanya vizuri na wimbo wake Aje, amekuwa msanii wa pili baada ya Davido kusainishwa kile wanachokiita ‘global deal’ na label hiyo iliyo nyumbani kwa wasanii wakubwa duniani.

Tuesday, 24 May 2016

Alikiba Awaomba Mashabiki Zake Wampigie Kura Diamond


 

Alikiba amewaomba watanzania kumpigia kura Diamond anayewania tuzo ya BET zitakazofanyika, Juni 26 Los Angeles, Marekani.


Wiki iliyopita Diamond alitangazwa kuwania tuzo ya BET kwa mara ya pili kwenye kipengele cha Best International Act: Africa akiwa ni msanii pekee kutoka Afrika Mashariki huku tuzo hiyo ikiwaniwa na wasanii wengine kama Wizkid, Yemi Alade, AKA, Cassper Nyovest, Black Koffie, MZVEE na Serge Beynaud.
Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Alikiba aliwaomba watanzania wampigie kura Diamond kwenye tuzo anazoshiriki za BET na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Tanzania kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.
“Of course nawasupport wote ndiyo, vote for Diamond kwenye tuzo za BET kwa sababu yeye ndiyo anayetuwakilisha,” alisema Alikiba.
Alikiba kwa sasa ni msanii aliye chini ya label ya Sony Music na wimbo wake mpya ‘Aje’ unafanya vizuri kwenye TV na Redio japo una siku tano tu tangu utoke, May 19.

Ali Kiba Ft. M.I - AJE | Lyrics/Mashairi

[Verse 1 – Alikiba]
Ucheshi na sauti
Amenifanya nam-miss tu
Mwambie asiogope
Ali ni kipenzi cha watu
Ntafanya party nyumbani
Hiyo yote kwa ajili yake
Tena asije peke yake
Asiogope aje na wenzake
Ntafanya party nyumbani
Hiyo yote kwa ajili yake
Tena asije peke yake
Asiogope aje na rafiki zake eh
[Chorus – Alikiba]
Basi mwambie aje (aje)
Oh aje (aje)
Aje na rafiki zake (aje)
Asije peke yake (aje)
Oh aje (aje)
Aje, oh aje (aje)
Aje jamani aje (aje)
Aje nam-miss aje (aje)
[Verse 2 – Alikiba]
Uzuri wake timilifu
Nshamuona na watu maarufu tu
Kina Wema Sepetu
Nikaomba namba bichwa akanishushua shuu!
Ilinikosesha raha
Lulu nae kamdanganya
Kwamba mi ni wa kwake
Aniogope tena asinichekee
Ilinikosesha raha
Lulu nae kamdanganya oh
Kwamba mi ni wa kwake
Aniogope tena asinichekee
[Chorus – Alikiba]
Basi mwambie aje (aje)
Oh aje (aje)
Aje na rafiki zake (aje)
Asije peke yake (aje)
Oh aje (aje)
Aje, oh aje (aje)
Aje jamani aje (aje)
Aje nam-miss aje (aje)
[Verse 3 – M.I]
I say, I say, I say…
I’m gonna marry you one day
Come through baby girl
I just want us to speak
See we met on a Monday
You must be next Monday
Cause you make it one week
Have you been to the West side?
Forget whatever you seen on them Nollywood films
I wanna be your best guy
So let’s try till you testify no one’s better than him
So baby, give me your digits
Let me google map location, come and visit
You should show up in something exquisite
I can come over to yours, girl, where is it?
You could teach me to speak in Swahili
Like “sawa sawa, mambo vipi?”
Can you tell that I’m feeling you really?
Alikiba and M.I, my baby, I know that you feel me
[Chorus – Alikiba]
Basi mwambie aje (aje)
Oh aje (aje)
Aje na rafiki zake (aje)
Asije peke yake (aje)
Oh aje (aje)
Aje, oh aje (aje)
Aje jamani aje (aje)
Aje nam-miss aje (aje)
[Outro]
Come through, baby
I want you to come through, baby
Come through, baby
I want you to come through, baby
Come through, baby
I want you to come through, baby
Come through, baby
I want you to come through, baby

Monday, 23 May 2016

BASATA Yatoa Baraka Zake Kwa Alikiba, Hivi Ndivyo Alivyojibu



Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA limempongeza Alikiba baada ya kusaini mkataba wa kimataifa na label kubwa duniani, Sony Music.
Sony-Alikiba
BASATA lilimpongeza Alikiba kupitia akaunti ya Twitter na kuelezea kuwa mafanikio hayo yamekuja kutokana na nidhamu aliyonayo.
“Tunampongeza Msanii Ali Kiba kwa kusaini mkataba na Kampuni ya Kimataifa ya Sony Music. Nidhamu, maadili & Sanaa ya staha hulipa,” waliandika BASATA
basata-3
Alikiba naye aliwashukuru Basata kwa kuandika: Nalishukuru @BasataTanzania kwa pongezi kwani nyinyi ni Kama wazazi katika sanaa yetu Asanteni sana proudly TZ.”
basata-4

 Bongo5.com

Sunday, 22 May 2016

Ali Kiba, Diamond Platnumz Kimenuka Hatari. Ipo Hapa

Kimenuka! Ndivyo unavyoweza kusema kufuatia mafahari wawili wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ na Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kudaiwa kutupiana vijembe vya kufa mtu baada ya kuwepo kwa madai ya Kiba kuhujumiwa.

Kwa mujibu wa chanzo makini, ili kuweka hujuma ya kibiashara, hivi karibuni, pamoja na kukanusha mara kadhaa kutokuwa na tatizo na Kiba, Diamond alidaiwa ‘kutengeneza’ kwa makusudi penzi la mwigizaji Jacqueline Wolper Massawe na msanii wa Wasafi Classic Baby (WCB), Rajabu Abdulhan ‘Harmonize’ kisha kuvujisha video ya uhusiano huo mpya siku ambayo Kiba alikuwa akiuachia wimbo wake mpya wa Aje (Jumamosi iliyopita), lengo likiwa kuhamisha upepo mashabiki kutoka kwenye wimbo mpya na kujali mapenzi ya wawili hao.

“Ni hujuma ya kibiashara, Diamond na uongozi wake wameamua kumfanyia Kiba ili wimbo wake ukose kiki kwa watu,” kilidai chanzo chetu.


VIJEMBE VYATAWALA
Hata hivyo, kwa mujibu wa mmoja wa mameneja wa Kiba ambaye hakupenda jina lichorwe gazetini, amemtupia vijembe Diamond kwa kudai licha ya hujuma hizo lakini hawawezi kumgusa Kiba.
“Wanajisumbua, kizuri huwa kinajiuza chenyewe na huwezi kuzuia mafuriko kwa mikono. Wameingiza kiki zao lakini msimu huu hazifui dafu. Wimbo (Aje) umepokelewa vizuri na una mafanikio makubwa hadi sasa.


AZUNGUMZIA MKATABA
“Kuonesha kwamba Kiba amekubalika, ndani ya muda mfupi baada ya wimbo huo kuruka hewani, amelamba mkataba na kampuni ya kimataifa ya Sonny Music. Sasa hapo ndipo utakapoona Ngoma ya Kiba imekubalika kiasi gani, hawamuwezi huyu,” alisema meneja huyo.

KEJELI SASA!
Kama hiyo haitoshi, meneja huyo alizidi kutupa vijembe kwa Diamond kwa kueleza kuwa Kiba ni mkongwe hivyo kamwe hawezi kulingana naye kimuziki.

“Diamond hamuwezi Kiba, ameanza kuimba wakati Diamond bado hajawa msanii. Ameshafanya mengi kwenye huu muziki kuliko huyo Diamond, unakumbuka dili la One 8, Kiba aliungana na mastaa wakubwa katika project iliyokuwa chini ya msanii mkali duniani, R-Kelly (Robert Sylvester Kelly), Watanzania wanajua,” alisema meneja huyo.

KIBA HUYU HAPA
Alipoulizwa Kiba kuhusiana na vijembe na kejeli hizo anazodaiwa kuzitupa kwa mpinzani wake (Diamond), alisema ishu hiyo isiitwe vijembe badala yake ieleweke kwamba ndiyo ukweli.
“Siyo vijembe wala majungu. Huo uliosikia ndiyo ukweli wenyewe,” alisema Kiba.
TEAM DIAMOND WAJIBU MAPIGO
Kupitia mitandao mbalimbali ya kijamii, wafuasi wa Diamond waliojipa jina la Team Diamond walicharuka kusikia msanii wao amehusishwa na hujuma za ‘kumuua’ Kiba kibiashara.
“Hana lolote huyo, Diamond ameshafanya makubwa sana ndani ya muda mfupi kumzidi yeye ndiyo maana anatapatapa kwa sababu nani asiyejua kuwa Diamond yupo fasta katika kuona fursa kuliko Kiba?
“Wolper na Harmonize wapo penzini kwa matakwa yao na si kwa kumuua Kiba, hana jipya,” aliandika mmoja wa wafuasi wa Diamond kwenye Mtandao wa Kijamii wa Instagram.


DIAMOND ANASEMAJE?
Jitihada za kumpata Diamond ili azungumzie suala hilo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kutopatikana hewani hadi tunakwenda mitamboni lakini meneja wake, Babu Tale alipoulizwa kuhusu suala hilo, alicharuka:

Risasi Jumamosi: Tale tuambie, hivi kuna ukweli wowote kwamba Diamond na timu yako mlipanga kumzima Kiba alipokuwa anatambulisha ngoma yake mpya kwa kutupia video inayoonesha uhusiano wa Wolper na Harmonize?

Tale: “Siyo kweli. Hilo swali ni la kipuuzi. Sikiliza, ngoja nikuunganishe na bosi wako ili asikie unavyoniuliza. Nakata halafu nakupigia.
Hata hivyo, Babu Tale hakufanya hivyo na alipopigiwa tena, simu yake haikupatikana.

WOLPER AFUNGUKA
Gazeti hili halikuishia hapo, lilimtafuta Wolper ili kujua kama ni kweli ametumika kumfifisha Kiba kimuziki ambapo alisema si kweli kwani penzi lake na Harmonize limetoka katika mioyo yao.
“Hakuna kitu kama hicho. Sisi tumependana wenyewe wala hatujashinikizwa na mtu yeyote kuvujisha penzi letu eti ili kumfanya fulani afifie! Kama imetokea limevuja wakati ambao huyo Kiba naye ametoa wimbo itakuwa tu imetokea lakini si kwamba tumedhamiria,” alisema Wolper huku simu ya Harmonize ikiita bila kupokelewa.

Ugomvi wa Diamond na Kiba ni wa muda mrefu ambapo huwa na msimu kwani kuna wakati unachachamaa kama sasa na kipindi kingine unapoa na hakuna anayejua hatima yao.

Chanzo: Global Publishers

Saturday, 21 May 2016

Kituo Maarufu Cha TV Huko Nigeria, Soundcity Yazindua ‘Alikiba Day’ Maalum Kwa Kiba



Pale kituo maarufu cha TV cha burudani nchini Nigeria kinapoamua kutenga siku maalum kwaajili ya Alikiba, ni dalili kuwa muimbaji huyo wa Aje amekinukisha mbayaa.
13258935_499902356886644_1938126692_n
Soundcity imeanzisha #AlikibaDay kwa heshima ya Alikiba ambapo neno hilo linaonekana kwenye screen ya TV kwa siku nzima.
13116579_1596499930679359_288692801_n
“We still counting down Major Announcements #4 : Exclusive ALIKIBA Day @SoundCityafrica Thank you @SoundCity kwa kumpa heshima hio ya kwanza kwenu kwa kudedicate channel yenu siku nzima kwa @officialalikiba Watanzania wenzetu wamefurahi sana 🇹🇿 #KingSoundCity #Rockstar4000 #SonyMusicAfrica #TheCountDownContinues,” ameandika meneja wake, Seven Mosha kwenye Instagram.
Wiki hii Alikiba ametengeneza vichwa vya habari Afrika nzima baada ya kusainishwa deal la kimataifa na label ya Sony Music. Pamoja na kusaini deal hilo, Kiba pia ameteuliwa kwenye kampeni ya Food Revolution ya taasisi ya Jamie Oliver Food Foundation.
Kupitia Instagram, Alikiba aliandika: Major Worldwide Announcement #3: I’m joining global master celebrity Chef Jamie Oliver and have partnered for an initiative I am very passionate and proud to be associated with. Proud to support Jamie Oliver and to come on board as a Global Champion and Global Ambassador for #FoodRevolution!”

BONGO5

Friday, 20 May 2016

Ukitoa mkataba na Sony Music, hii ni dili ya pili AliKiba (@OfficialAliKiba) amepata, zipo zingine 5



News
Huu ni mwaka wa Alikiba. Baada ya kusaini mkataba mnono na Sony Music itakayomshuhudia akienda rasmi kimataifa, staa huyo amepewa dili jingine la kufanya kazi na taasisi ya Jamie Oliver Food Foundation.
Trace Urban wameshare habari hiyo kwenye Twitter. “This is .@OfficialAlikiba’s year! He has a dope partnership w/the #JamieOliverFoundation too.”
kiba22
Taasisi hiyo ya kimataifa inajihusisha na masuala ya chakula na upishi. “Access to good, fresh, real food and the basic skills to cook it has the power to transform lives, and that is what the Jamie Oliver Food Foundation is all about,” imeandika kwenye tovuti yake.
Taasisi hiyo inafanya kazi Uingereza, Marekani Australia na hutoa mafunzo mbalimbali kuhusu chakula. “Our food education programmes in schools, communities and with groups of vulnerable young adults teach people about food, where it comes from, how it affects their bodies and how to cook it.”
feature-header23
Taasisi hiyo ilianzishwa na mpishi maarufu wa Uingereza, James Trevor Oliver
Katika hatua nyingine mkataba wa Alikiba na Sony utamwezesha kufanya collabo na msanii wa Marekani aliye chini ya label hiyo pia.
“@SonyMusicAfrica will have USA/East Africa collaboration for
@OfficialAlikiba with other #Sony artists,” wametweet Trace.
Habari hii kutoka http://www.bongo5.com

Ali Kiba (Official Video) - AJE | Download Mp4

Ali Kiba his new video title AJE, Watch and Download video down here

Audio | Ali Kiba - AJE (Official) | Mp3 Download

Hii hapa AUDIO rasmi ya nyimbo ya ALI KIBA, katika AUDIO hii M.I kutoka NIGERIA hajasikika, Kuwa wakwanza kuipakua hapa:

Kama umemiss kuangalia video ya AJE, Bonyeza hapa Chini kuidownload:

 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes