BREAKING NEWS
Showing posts with label Entertainment. Show all posts
Showing posts with label Entertainment. Show all posts

Monday, 18 July 2016

Mwaimbaji Shaa Hayupo Tena Katika Lebo Hiyo Inayomilikiwa na Master Jay

Malikia wa uswazi kama mwenyewe anavyopenda kujiita Shaa ameweka wazi zile tetesi zilizokuwa zimezagaa kwamba ameondoka Mj Record na kesema ni kweli hayupo chini ya lebo hiyo lakini haimaanishi kwa hafanyi kazi na studio za Mj .

Hata hivyo Shaa amesema ameanzisha kampuni yake inayoitwa SK ambayo ni matokeo ya kazi za sugua gaga,toba na nyingine ambazo zilirudisha gharama za Mj na kumuwezesha kufungua kampuni hake hiyo binafsi ambayo anatarajia kusajili wasanii hata wa tano ila kwa sasa yupo yeye peke yake.

Hata hivyo Shaa ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Sawa kupitia kampuni yake hiyo ila unaambiwa Shaa hayupo taari kuyazungumzia mahusiano yake kama ailivyo mpenzi wake Master J ambaye akiulizwa na huwa anajibu lakini kwa Shaa nitofauti kabisaa

Nahreel Alinitengenezea Hit Yangu ya Kwanza Afrika, Siwezi Kuacha Kufanya Naye kazi – Jux

Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa wasanii wengi waliokuwa wakifanya kazi na Nahreel wakiwemo Weusi wameikimbia studio yake ya The Industry baada ya kubadilisha utaratibu wa kurekodi nyimbo.

Jux kwa upande wake amekanusha na kudai kuwa Nahreel bado ni mshkaji wake mkubwa na mwishoni mwa wiki walikuwa pamoja. Anadai kuwa bado ana kazi nyingi kwa producer huyo na kwamba wakati mwingine huamua kubadilisha ladha ili kuogopa nyimbo zake kuzoeleka.

“Nahreel mimi amenitolea hit song, amenitolea ‘Looking For You, naweza kusema ndio wimbo ambao hata Kiafrika ndio ilifanya poa sana,” Jux ameimbia Bongo5.

“Hata kuna wasanii wakubwa wa Kiafrika wengine ambao siwezi kuwasema sasa hivi wameiskia na wameniona huku na tunakuja kufanya nao nyimbo baadaye, ni sababu ya Looking For You. Nisingetoka kwa Bob labda nisingepata kitu tofauti,” amesisitiza.

Kingine amedai kuwa muda wote huu hakuwepo alikuwa nchini China na pia Nahreel amekuwa na miradi yake mingine mingi ikiwemo kwenda Afrika Kusini kufanya video za Navy Kenzo na za wasanii wa The Industry.

“Karudi, tumekutana jana, bado mshkaji wangu na bado nafanya naye kazi pia, sababu ya yeye kubadilisha utaratibu wa studio mimi haijaniathiri chochote kwasababu ni program zake yeye mwenyewe alizotaka kufanya, kwahiyo mimi naona ni sawa. Kwanza mimi ni mmoja wa watu niliyeona hivyo yaani Nahreel alikuwa anadeserve hicho kitu pia kwasababu alikuwa anafanya kazi sana.”

Wiki iliyopita Jux aliachia wimbo wake mpya, Wivu aliorekodi kwenye studio za AM Records.

Bongo5

Wema Sepetu na Idris Sultam Wamwagana Rasmi

DAR ES SALAAM: Ubuyu wa motomoto wa mjini ni kwamba, zile mbwembwe zote za penzi la mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Idris Sultan, zinadaiwa kufikia ukingoni na sasa imebaki stori kwani Wema, Idris wamwagana rasmi.

Wikienda limeng’atwa sikio kuwa, kitendo cha wawili hao ‘kushoo lavu’ kwenye ile Pati ya Black Tie iliyofanyika juzikati katika Ukumbi wa King Solomoni pale Namanga, Dar ilikuwa ni geresha tupu kwani walishamwagana kitambo.

Hata hivyo, kama utakumbuka au hukuipata ni kwamba iliwahi kuvujishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema na Idris wamemwagana lakini baadaye zilivunjwa picha zikiwaonesha wakiwa wameshikana mikono na mahaba tele ili kuua soo.

wema-na-idriss-insta Sasa ubuyu ulionyooka kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao unadai kwamba, kilichotokea kwenye pati hiyo zilikuwa ni mbwembe za kuzuga zilizotokana na huruma ya Idris.

Ilidaiwa kwamba, Idris alilazimika kufika kwenye sherehe hiyo kwa sababu ilishatangazwa kuwa atakuwa ni miongoni mwa ‘ma-hosti’ lakini ukweli ni kwamba mambo yalishaharibika.

wema na idris 2“Unajua watu wengi hawakujua kuwa Wema na Idris walishaachana kitambo na pale (King Solomoni) walikuwa wanafanya maigizo tu, japokuwa haijulikani moja kwa moja sababu ya kuachana kwao lakini Wema anadaiwa kuwa tatizo kwa Idris kutokana na kutokea kwa migogoro ya kila kukicha,” alitonya sosi huyo.

Hata hivyo, katika kuonesha kwamba kuna kitu kinaendelea, wana-ubuyu wetu walifuatilia akaunti zote za mastaa hao katika mitandao ya kijamii kuona kama mbwembwe zao zinaendelea na kubaini kuwa hawako sawa baada ya kusoma ujumbe wa Wema unaoonesha kumbembeleza Idris huku jamaa huyo akionesha wazi kuwa hakuna mapenzi bali ni drama tu.

Ili kuleta ushahidi, tunakukaribisha hapa kusoma nukuu zao mtandaoni;

MANENO YA WEMA
“Having you as a friend, a brother, a lover and of course a shoulder to cry on every time, i’m at my worst has been the best feeling ever… I wouldn’t want to lose this feeling over anything…
“I realized without u then i ain’t complete…. You have stood by me in good times and bad and even when i messed up so bad you would look me in the eyes and tell me, “Baby, its okay, we gona fix this”…
“Idris you have been one of a kind and losing u is the last thing i want on this earth… I will love you until forever, until death do us part we will be together…
“I will hold on to you till da last minute because together we will get there…. I love you with my life…. For I believe you are my true love, my baby and inshallah! The Man that my kids will call daddy…” alimalizia kuandika Wema akimlilia Idris.

IDRIS NAYE ALIANDIKA:
“Kumbuka kurekebisha kiatu kila hatua ya maisha unayopiga kisije kuchomoka ukakanyaga mwiba ukapunguza spidi.”

WEMA ASAKWA
Wikienda halikuishia hapo kwani lilimsaka Wema anayedaiwa kubwagwa, alipopigiwa simu hakupokea, akaandikiwa ujumbe mfupi wa sms ambao pia hakuujibu.
Pia alitumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp lakini pia hakujibu.

 UBUYU WAKAMILIKA KWA IDRIS MWENYEWE
Wikienda liligeuza dira yake na kuielekeza kwa Idris ambaye alifunguka bila kuacha lolote.
Kwa mujibu wa Idris, yeye na Wema walishasahau kuwa waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwani kwa sasa kila mtu ana ‘biashara’ zake.

“Mimi nilikwenda kwenye ile pati kwa sababu ya kuwaonea huruma tu kwani ndiyo kwanza wameanzisha kampuni na mbaya zaidi walikuwa wakiniweka kwenye matangazo. Unadhani watu wangewachukuliaje? Sikutaka kuwaharibia shoo lakini mimi nilishaachana naye na nina biashara zangu nyingine,” alifunguka Idris.

Idris alienda mbali zaidi na kusema kuwa kwa sasa ana mwanamke mwingine anayempenda na siku si nyingi mambo yakikaa sawa, atamuanika.
“Mwenzenu nina kifaa kingine soon nitawafahamisha,” alisema Idris.

WEMA NA IDRIS
Awali Wema na Idris walificha uhusiano wao lakini baadaye waliamua kujiachia ambapo mlimbwende huyo alidai kushika ujauzito lakini kwa bahati mbaya ukachoropoka.

Source:Global Publishers

Huu ndiyo ukweli kuhusu ndoa ya siri ya D’Banj

D’Banj bado hajafunga ndoa ila amemtambulisha mchumba wake kwa wazazi wake na familia yake pekee – kwa mujibu wa chanzo cha habari.

Mapema mwezi huu zilienea taarifa kuwa staa huyo wa muziki kutoka Nigeria, amefunga ndoa na msichana anayedaiwa kuwa na asili ya Afrika Kusini na Nigeria lakini makazi yake ni nchini Marekani, Didi Kilgrow.
Akiongea na Sunday Scoop mtu wa karibu wa D’Banj amesema, “Dbanj has given so much information about himself to the public and he deserves to keep some things private and this is one of those things.”
“He is not worried about losing female fans, he just wants his marriage and the impending white wedding off public radar,” ameongeza mtu huyo.

Kajala Achefua Watu Baada Ya Kuvaa Nguo Inayoonyesha Matiti Yake

KAJ


Kajala Masanja; Bongo Movie Actres Kajala Masanja looks faboulous on new photos of the day

Tuesday, 5 July 2016

Alikiba Afungua Brand Yake Ya Nguo...!

Ali Kiba ameamua kuja na Brand yake ya kofia za AK alikiba kwa ajili ya mashabiki zake na watu wake wa karibu.
Ak(alikiba)👑 New brand cap available..30k
For more information check:0654 367910 or 0652 988888

Monday, 4 July 2016

Darasa Afunguka Kuhusu Ishu ya Linah Kutamani Kuwa Naye, Adai ‘Nina Mpenzi’


Mkali wa Hip Hop Bongo, Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’ amefunguka kuwa anaheshimu maneno ya msanii mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kuwa anamkubali na kutamani kuwa na mwanaume mwenye sifa kama zake lakini yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu.
Akizungumza na Wikienda alipotembelea Global TV Online wikiendi iliyopita, Darasa alisema kuwa Linah ametumia ujasiri kutoa hisia zake na amefurahi kusikia anamkubali ingawa yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu na wanaaminiana.
“Namshukuru kwa kunikubali, kiukweli namheshimu na nimefurahi,” alisema Darasa.
Darasa alifunguka hayo baada ya hivi karibuni Linah kueleza hisia zake kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatamani awe na mwanaume mwenye sifa alizonazo Darasa.
Share na Marafiki:

Saturday, 2 July 2016

Wema Sepetu ‘Mimi Dhahabu Inayogombewa na Watu, Sijali Wanaonichafua’


WemaSepetu

Mrembo wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, amesema yeye ni dhahabu inayogombewa na watu hivyo hajali hata kama atachafuliwa namna gani katika mitandao ya kijamii.
Wema aliliambia MTANZANIA kwamba, hana mpango wa kujibu vibaya vinavyoongelewa kuhusu yeye kwa kuwa yeye bado ni dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu.
“Mimi ni kama dhahabu hivyo kila mtu anatamani kuishika, watu wanaacha kufanya yao kila siku Wema, kwa sasa niko na mambo yangu ya kutafuta fedha sina habari na mtu hata aniandike vibaya vipi,” alisema Wema.
Aliongeza kwamba licha ya kusemwa, amezidi kujiongezea mashabiki na mikataba mbalimbali ya kufanya kazi na makampuni yenye majina makubwa kwa kuwa yeye ni kama dhahabu isiyochafuka.

Share na Marafiki: 

Abdu Kiba adai wasanii wa WCB wanabebwa na Promo

Abdu Kiba amesema kuwa promotion ndiyo inawabeba wasanii wa lebo ya WCB.Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM, “Sijafikiria kuimba na msanii kutoka WCB, kwa sababu sijaona anayeimba type ya muziki wangu.”
“Hata kama wana promote kwa sababu ndiyo walipoona wao ndiyo wanaweza wakafanya na watu wakaweza kuelewa lakini siku zote ajuae hazami,” alisema Abdu Kiba.
Aidha aliongeza kuwa bado hajaona msanii anayeimba type ya muziki wake ndani ya lebo hiyo [WCB].
Hata hivyo mapema mwezi huu msanii huyo alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha EA Radio kuwa yupo tayari kujiunga na lebo wa WCB kama watakubaliana na kuweka hela mezani kauli ambayo baadaye yeye mwenyewe aliipinga kuwa watu hawakumuelewa vizuri alichomaanisha

Chris Brown aingia tena matatani huko Ibiza

Chris Brown ameendelea kucheza na mdomo wa sheria kwa kufanya uharibufu wa nyumba huko Ibiza.
chris-brown-ibiza
Staa huyo alikodi nyumba moja wiki iliyopita huko Villa, Ibiza alipokwenda mapumzikoni akiwa na watu wake. Mwenye nyumba hakuridhishwa na muonekano wa nyumba yake baada ya msanii huyo kumaliza muda wake wa kukaa kwenye nyumba hiyo.
Mwenye nyumba pia amedai kuwa amekuta ukuta wa nyumba yake umechafuliwa vibaya huku kukiwa kumefanyika uharibifu mkubwa ndani ya nyumba yake hiyo na hivyo ametaka kulipwa kiasi cha dola 60,000 kutokana na uharibifu huo uliofanywa na Chris Brown.
Wiki iliyopita Chris Brown alishtakiwa na aliyekuwa meneja wake, Mike G kwa madai ya kumpiga ngumi usoni na shingoni bila hata kumfanya kitu.

Alikiba Atambua Kiu ya Mashabiki Zake, Asema Haya

Alikiba amesema anaamini mashabiki zake mpaka sasa watakuwa na kiu ya kusikiliza kazi mpya kutoka kwake hivyo hata waangusha kwani kwa sasa yeye atakuwa akitoka kazi juu ya kazi ili aende sawa na mashabiki zake.

“Ukiwa kama shabiki yangu number moja click link kwenye Bio yangu kufikisha 2 Million Views. Kisha baada ya hapo wewe shabiki yangu una haki ya kunidai mashine nyingine. Najua fika una kiu ya kusikia nini nimekuandalia. Asikwambie mtu ni mkwaju juu ya mkwaju. Twende sawa ila tusisahau ibada.” alisisitiza Alikiba

Friday, 1 July 2016

Namchukulia TID Kama Kaka Yangu, Nampenda, Namheshimu – Billnass

Kuna vita vikali vya maneno kati ya TID na aliyekuwa kijana wake, Billnass.
13437329_638034583012192_71100538_n
Katika mahojiano mengi aliyofanya, Mnyama anaonekana kukerwa na kitendo cha rapper huyo wa Chafu Pozi kuondoka kinyemela Radar Entertainment – label iliyomtoa. Anaamini kuwa Bill ni mtu mwenye tamaa na hayupo real na kwamba alimtumia tu kupata jina na baada ya kufanikiwa kamtema kama ganda mua!
Hata hivyo Bill ambaye jina lake halisi ni William, haoneshi kutaka kumjibu TID, hataki makuu na ‘anaplay smart.’
“Kuna vitu vingi sana ila mimi sitaki kuzungumza sana, ninachoweza kusema ni kuwa nampenda TID na namheshimu,” rapper huyo alikiambia kipindi cha Super Mega cha Kings FM kinachoendeshwa na Divine Kweka.
Bill bado anasisitiza kuwa mkataba wake, hata kama ulikuwa wa maneno ulimalizika baada ya mwaka mmoja na alikuwa huru kwenda popote. Anasema hawezi kuongea na TID moja kwa moja lakini ameshaongeza na watu anaowaheshimu ili waongee na bosi wake huyo wa zamani ili wayaache yaliyopita yapite na wasichafuliane kwenye vyombo vya habari.
Msikiliza hapo chini.

Diamond Platnumz Aweka Picha Ya Alikiba Kwenye Ofisi Yake, Itazame Hapa...!

Meneja wa Diamond, Babu Tale ameonyesha kuwa wao hawana tatizo na Alikiba baada ya kupost kipande cha video kinachoonyesha picha ya msanii huyo ndani ya studio ya Wasafi Records.
Bongo
Ni muda mrefu imezungumzwa kuwa Diamond na Alikiba wana bifu mpaka kupelekea kuanzishwa kwa baadhi ya team za mitandaoni za kukejeli mafanikio ya msanii wa team nyingine lakini hiyo ni dalili kuwa ipo siku itabaki historia tu.
Babu Tale alipost kipande hicho cha video kinachoonyesha baadhi ya picha za wasanii wakubwa Bongo akiwemo Marehemu Bi Kidude, Mr Blue, Dully Sykes, Juma Nature, Q Chief, Alikiba na wengine wengi.
Je, hiyo inaweza ikawa ndiyo kiki ya kuikaribisha video ya wimbo mpya wa Diamond aliowashirikisha P Square ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni?
Tazama video hapa.

Thursday, 30 June 2016

CHID Benz Afunguka ya Moyoni..'Dawa za Kulevya Sitaki Hata Kuzisikia Zimeniumiza Sana na Kunidhalilisha Sana'



“Dawa za kulevya kwangu zinabaki kuwa historia, sitaki hata kuzisikia zimeniumiza sana kimawazo, zimenidhalilisha na zimepoteza mwelekeo wa maisha yangu, sina hamu nazo tena nina hasira nazo siwezi kuzirudia kwa sasa naangalia maisha yangu mapya katika muziki,” - Chid Benz.

Tupia neno moja la kumtia moyo

TAZAMA Nyumba Aliyokuwa Anaishi Mtangazaji Millard Ayo Kabla Mambo Hayajamyookea...




TBT mtu wako wa nguvu nikiwa nje ya chumba nilichokua naishi kwa miaka mitatu 2005-2008 Keko Machungwa Dar es salaam toka wakati naanza kazi ya Utangazaji/Uandishi kwenye Radio na Gazeti la #MsemaKWELI Hakijawahi kuwa na umeme kwa miaka yote, pamoja na yote sikuwa na neno kuishi hapa... jirani yangu alikua Bwana @yonathanlanda ndio mambo ya kupasi, kuchaji simu na kuangalia TV nilikua nilimalizana nayo kwake, tusikate tamaa watu wangu, kama una nia... hapo ulipo unapita tu.

Floyd Mayweather ni mshkaji wangu, tunaongea sana – Prezzo

Mfalme wa bling bling nchini Kenya, Prezzo amedai kuwa bondia tajiri wa Marekani, Floyd ‘Money’ Mayweather ni mshkaji wake na huwa wanapiga story za hapa na pale.
Prezzo1
“Mimi nina connection, mimi na Floyd Mayweather yule bondia mimi na yeye tunaongeaga yaani,” Prezzo alikiambia kipindi cha Funiko Base cha Radio 5 ya Arusha.
“Fight yake sio ile iliyopita, ya mwisho, ile fight yake ya 48 alikuwa amenialika shida ilitokea kwamba nilikuwa sijarenew visa yangu ya America na huwa kuna bonge la foleni, so siku yeyote nikienda Las Vegas usishangae kuniona mimi na Mayweather tunakamua yaani full makamuzi na tena kwa mara nyingine hiyo ndio tofauti yangu na huyo jamaa anaitwaje tena?” alijitapa rapper huyo.
Msikilize hapo chini.

Hii Ndio List ya Mastaa wa Tanzania Waliokuwa Verified Instagram


Kuwa verified katika mitandao ya kijamii ni kitu ambacho kinawaongezea wasanii umakini na kuwapatia uhakika kwa mashabiki wao, Kwa Tanzania idadi ya wasanii inazidi kukua ikiwa ni June 29 2106 mkali wa bongofleva Baraka Da Prince amekuwa miongoni mwa wasanii waliokua verified kwenye mtandao wa Instagram.
Msanii huyu mwenye followers laki tatu na arobaini na nne elfu na kuweza kuwa miongoni mwa wasanii wa kitanzania waliokua verified, wasanii hawa kama Flaviana Matata, Diamond Platnumz, Vanessa Mdee, Idris Sultan, Ommy Dimpoz na Ali Kiba.
barakalist ya mastaa wengine waliokua verified hii hapa chini
1.Diamond Platnumz
mond

2. Vanessa Mdee
vee money
3. Flaviana Matata
matata
4. Ommy Dimpoz
ommy dimpoz
5. Idris Sultan
idris sultan
6. Ali Kiba
Ali K


Share na Marafiki: 

Friday, 24 June 2016

Chidi Benz"Wadau Wa Muziki Ni Chanzo Cha Wasanii Kutumia Unga"

Msanii wa muziki wa Hip Hop, Chidi Benz amefunguka na kueleza jinsi wadau wa muziki nchini wanavyosababisha wasanii wa muziki kuingia kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya.
Chidi
Chidi Benz
Rapper huyo ambaye ameachana na matumizi ya Madawa ya kulevya hivi karibuni, ameiambia BBC kuwa wasanii wengi wanaingia kwenye Madawa ya kulevya baada ya kupata stress za kubaniwa kwenye muziki.
“Watu wanamsongo wa mawazo, mashabiki wetu hawajui sisi jinsi tunavyodeal na watu ambao wanatufikisha kwao, wadau wa muziki, wadau wa muziki ni watu tofauti sana na wanafanya vitu vibaya sana,” alisema Chidi. “Wachache wapo wanaosaidia vizuri, lakini ni wengi wanaoharibu na wanaharibu sana sana, yaani mtu anakuwa na kisasi na wewe na yupo tayari kukufanyia kitu chochote, akushushe, akupinguze mpaka umalize pesa zote na usipingwe hata wimbo wako mmoja,”
Pia rapper huyo alisema wasanii wengi wanabaniwa kutokana na migongano ya kimaslahi katika kazi au kushare mademu na wadau wa muziki.
“Huu muziki tunaoufanya na haya maneno tunayoyaimba, kuna wale ambao wanachukulia starehe na kuna wengine wanachukulia unawasema au mabinti zao wanatupenda sisi wasanii. Unakuta kuna binti amekupenda wewe msanii, kumbe yule ana mtu mwingine au mdau, sasa huyo mtu akisikia kwamba Chidi Benz anadeal na mtu wake, hawezi kuelewa kwamba mtu wake ndio anamfuata Chidi Benz, ila yeye atakufanya kitu chochote kile ili akuumize au akuharibu na ‘akustopishe’ maendeleo yako. Na inawezekana yule mtu wewe haukudeal naye ila anakupenda tu kishabiki na anawaambia marafiki zake hivyo lakini marafiki zake inatokea wakaibadilisha na wakaiweka kimapenzi, tayari una vita na mtu wake ambaye anamwangalia,” alisema Chidi.
Pia rapper huyo amedai kilichomwingiza yeye kwenye matumizi ya Madawa ya kulevya ni kutochezwa kwa ngoma zake kwenye redio na runinga hali ambayo ilimfanya ajione mpweke

Friday, 17 June 2016

Mwasiti kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha Chidi Benz



Kama umemiss sauti ya Chidi Benz, kuna habari njema.
Mwasiti
Mwasiti anatarajia kuachia ngoma mpya aliyomshirikisha rapper huyo. Amesema huo ni wimbo waliofanya kitambo lakini ulikuwa bado kwenye makabati.
Akiongea na 255 ya XXL kupitia Clouds FM, Mwasiti amesema wimbo huo uliorekodiwa miaka miwili iliyopita unaitwa ‘Wanipa Raha’ na kwamba ni bonge la ngoma. “Ni kazi nzuri ambayo huwezi kusema imerekodiwa miaka miwili au mitatu iliyopita utasema ni ngoma ambayo imerekodiwa jana labda kwasababu ni kazi nzuri sana,” amesema Mwasiti.
Amesema wimbo huo umetayarishwa na Tudd Thomas.
Mashabiki wengi wameimiss sauti ya Chidi ambaye hivi karibuni alipelekewa Bagamoyo kwenye kituo cha kusaidiwa waathirika wa madawa ya kulevya.
13473220_636609463169591_1612920495_n
Ametoka na wiki hii ameonekana kwenye picha mpya akiwa ameanza kurejea kwenye afya yake.

Vanessa Mdee kuwania tuzo ya msanii bora wa kike wa Afrika katika tuzo za NEA Awards 2016



Mkali wa wimbo ‘Niroge’, Vanessa Mdee amechaguliwa kuwania tuzo ya msanii bora wa kike wa Afrika katika tuzo za NEA Awards 2016 za nchini Nigeria.
Vanessa
Muimbaji huyo amekuwa ni msanii pekee wa Tanzania aliyechaguliwa kuwania tuzo hizo huku Kenya ikiwakilishwa na Victoria Kimani katika kipengele hicho hicho.
Wasanii wengine anaoshindana nao katika kipengele hicho ni, Efya Ghana, Lira (SA), MZ Vee (GH), Sheebah Ndiwanjawulo (UG), Adiouza (SN) Knowless Butera (RW).
Aidha msanii bora wa kiume wa Afrika/ Nje ya Nigeria, kundi la wasanii wa Kenya, Sauti Sol linachuana vikali na wasanii wengine kama Stonebwoy na Sarkodie wote wa Ghana
Hi ndiyo list nzima.
Best Album
Y.A.G.I (Lil Kesh)
Applaudise (Iyanya)
Eyan Mayweather (Olamide)
Ghetto University (Runtown)
R.E.D. (Tiwa Savage)
Stories that Touch (Falz)
Seyi or Shay (Seyi Shay)
Mama Africa (Yemi Alade)
Wanted (Wande Coal)
Hottest Single
Oshinachi (Humblesmith)
Duro (Tekno)
Baba Nla (Wiz Kid)
Lagos Boys (Olamide)
Mama (Kiss Daniel)
Jagaban (Ycee)
Best Song
Pick Up (Adekunle Gold)
Oluwa Ni (Reekado Banks)
Vow (Timi Dakolo)
You Suppose know (Bez)
Type of Woman (Iyanya)
Go On (Niyola)
​Best Collabo
Moniegram (Mr. 2Kay ft. Timaya)
Romantic (Korede Bello ft. Tiwa)
My Woman, My Everything (Patoranking ft Wande Coal)
Yaya Oyoyo (Lil Kesh ft. DaVido)
Reggae Blues (Harry Song ft Others)
Your Number (Ayojay ft. Fetty Wap)
Sekem (MC Galaxy ft Swizz Beats)
Finally (Masterkraft ft. Sarkodie, Flavour)

Best Live Performer
Omawumi
Tuface
Solidstar
Yemi Alade
Dbanj
MC Galaxy

Best Music Video
Emergency (Dbanj Dir. Unlimited LA)
Right Now (Seyi Shay Dir. Meji Alabi)
Condo (Kuammy Dir. Moe Musa)
Karishika (Falz Dir. Aje Films)
Duro (Tekno Dir. Patrick Elis)
If I Start to Talk (Tiwa Dir. CP)
Quality (Pasuma Dir. HG2)
Sisi (Sexy Steel Dir. Chad Tennies)

African Male Artist (Non Nigerian /Africa)
Stonebwoy (GH)
FA (LIB)
Sarkodie (GH)
Sauti Sol (KQ)
Deng (LIB)
Papa Denis (KQ)
Bisa Kdei (GH)
Eric Geso (LIB)
Shattawale (GH)

African Female Artist (Non Nigerian /Africa)
Vannessa Mdee (TZ)
Efya (GH)
Lira (SA)
MZ Vee (GH)
Sheebah Ndiwanjawulo (UG)
Adiouza (SN)
Victoria Kimani (KQ)
Knowless Butera (RW)
 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes