BREAKING NEWS
Showing posts with label Chris Brown. Show all posts
Showing posts with label Chris Brown. Show all posts

Saturday, 2 July 2016

Chris Brown aingia tena matatani huko Ibiza

Chris Brown ameendelea kucheza na mdomo wa sheria kwa kufanya uharibufu wa nyumba huko Ibiza.
chris-brown-ibiza
Staa huyo alikodi nyumba moja wiki iliyopita huko Villa, Ibiza alipokwenda mapumzikoni akiwa na watu wake. Mwenye nyumba hakuridhishwa na muonekano wa nyumba yake baada ya msanii huyo kumaliza muda wake wa kukaa kwenye nyumba hiyo.
Mwenye nyumba pia amedai kuwa amekuta ukuta wa nyumba yake umechafuliwa vibaya huku kukiwa kumefanyika uharibifu mkubwa ndani ya nyumba yake hiyo na hivyo ametaka kulipwa kiasi cha dola 60,000 kutokana na uharibifu huo uliofanywa na Chris Brown.
Wiki iliyopita Chris Brown alishtakiwa na aliyekuwa meneja wake, Mike G kwa madai ya kumpiga ngumi usoni na shingoni bila hata kumfanya kitu.

Monday, 30 May 2016

Wizkid Apewa Shavu Na Chris Brown, Amuongeza Kwenye ‘One Hell of A Nite Tour’ Ulaya

Wizkid tayari anaishi ile ndoto ambayo wasanii wengi wa Afrika bado wanaiota. Kutoka kushirikishwa kwenye wimbo wa Drake ‘One Dance’ uliopo kwenye album Views na ulioshika namba moja kwenye chart za Billboard 100, hadi sasa kuongezwa kwenye orodha ya wasanii watakaomsindikiza Chris Brown kwenye ziara yake ya ‘One Hell of A Nite Tour’ barani Ulaya.
13248976_820765204721577_268213544_n
Taarifa hiyo ilitolewa na Chris Brown mwenyewe kwenye akaunti yake ya Instagram kabla ya Wizkid naye kuandika: 5th – 11th June I’ll be supporting my brother @chrisbrownofficial !! Get ur tickets!! #Onehellofanitetour Bringing the African wave!!”
Wizkid ana wimbo aliomshirikisha muimbaji huyo wa Marekani mwenye mashabiki wengi.

Friday, 20 May 2016

Audio | Chris Brown - Str8 Shots + Pop It | Mp3 Download


Download two tracks from Chris Brown, Str8 Shots and Pop It, Enjoy good music


 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes