BREAKING NEWS
Showing posts with label Kajala. Show all posts
Showing posts with label Kajala. Show all posts

Friday, 1 July 2016

Kajala Aeleza Mzimu wa Kifo Unavyomtesa

Msanii maarufu wa filamu Bongo, Kajala Masanja amefunguka kuwa, maisha yake ya sasa hayajatawaliwa na furaha kwani anaona kama vile siku zake za kuishi duniani zinakaribia kuisha.
 Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Kajala alisema kuwa amefikia hatua ya kusema hayo kwa kuwa, kila wakati moyo wake unamuenda mbio na wakati mwingine kukumbana na ndoto mbaya zinazomfanya aogope.

“Niseme tu kwamba sina amani kwa sasa kwani nakiona kifo changu, nikilala usiku nasumbuliwa na mzimu wa kifo, nikitaka kusafiri moyo unanilipuka, nahisi itakuwa ndiyo safari yangu ya mwisho, wakati mwingine naahirisha safari kwa hofu.

“Nikiumwa kidogo tu nakosa amani kabisa, naona kama vile sitapona kikubwa namuomba Mungu aniondolee hali hii ndiyo maana nimekuwa mtu wa ibada muda mwingi,” alisema Kajala.

Sunday, 5 June 2016

Kajala Amwanika Bwana Mpya!

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, staa wa filamu Bongo, Kajala Masanja juzikati alimwanika bwana’ke mpya, kufuatia kupigana kibuti na Mbongo Fleva, Quick Raca, Risasi linakujuza.

Kajala (picha ya kushoto) na mwamme anayedaiwa kuwa bwana wake mpya
Katika Pool Party ya staa mwenzao, Shilole, iliyofanyika katika uwanja wa ofisi ya BKT iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam, Kajala alimtambulisha mwanaume huyo bila kumtaja jina, akisema ndiye mtu wake rasmi kwa sasa.

“Naona unanitolea macho na kunitamani muda mrefu na unavyopenda umbeya unataka kujua hawa nilionao ni kina nani, naomba ufahamu kuwa huyu ndiye mchumba wangu wa sasa, ndiyo maana unaniona niko naye,” alisema msanii huyo.

Kajala, ambaye pia alimuonya bwana’ke huyo kuwa makini na paparazi wetu, alithibitisha usemi huo baada ya kuondoka pamoja na mtu wake huyo katika viwanja hivyo kuelekea Coco Beach kabla ya baadaye kuonekana tena pamoja wakinywa kinywaji kimoja ndani ya Ukumbi wa Club Billicanas.

Kabla ya kuwa pamoja na Quick Raca, Kajala alikuwa na mumewe, Faraji Chambo ambaye alihukumiwa kifungo cha miaka saba gerezani, Machi 2013 baada ya kupatikana na hatia ya utakatishaji pesa, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi wa Kisutu.

Chanzo: GPL
 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes