BREAKING NEWS
Showing posts with label Babu Tale. Show all posts
Showing posts with label Babu Tale. Show all posts

Saturday, 4 June 2016

Babu Tale: Wasanii Wa ‘WCB’ Wana Nyota Ya Kupata Wanawake Wenye Umri Mkubwa Zaidi yao (Video)

Baada ya kambi ya WCB kuonekana wasanii wake wanapenda kutoka kimapenzi na wanawake wenye umri mkubwa zaidi yao, uongozi wa kambi hiyo umelizungumzia swala hilo.Diamond, Harmonize
Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii, Mmoja kati ya viongozi wa juu wa kambi hiyo, Babu Tale, amesema ni bahati kwa wasanii wake kupata wanawake waliowazidi umri.
“Sisi tunameneji wasanii hatumeneji hisia zao, lakini ikitokea msanii fulani amempenda mwanamke fulani tunamuacha kwa sababu ni mapenzi yake,” alisema Tale. “Tunaona ni bahati kwa wasanii wetu kupata wanawake waliowazidi umri, hiyo ni bahati (anacheka) kwa sababu wanamuenzi Mtume Muhammad (s.a.w.w.) alimuoa Bi Khadija ambaye alimzidi umri,”
Hata hivyo, Tale alisema ndani ya WCB hawameneji mapenzi bali wanammeneji msanii pamoja na kazi zake.

Wednesday, 1 June 2016

Babu Tale Alimtelekeza Chidi Benz Sobber House - Mkuu wa Kituo


Akizungumza na E news ya East Africa Tv mkuu wa Bagamoyo sobber house amesema chanzo cha Chidi Benz kuondoka kwenye kituo chao ni kutelekezwa na waliompeleka.

Anasema tangia Chidi apelekwe pale hakukuwa na huduma zozote zinazotumwa kama walivyokubaliana na kila walipokuwa wanamtafuta Babu Tale hakuwa tayari kupokea simu wala kutoa ushirikiano.

Anasema pia kukosekana kwa vitu muhimu ndio vilifanya Chidi aondoke na wala hakutoroka.

Japo Sijajua ni vitu gani walikubaliana awe anapeleka.


My take, kama ni kweli hii ishu basi Tale amekosea sana hakufanya uungwana. Ni kama kamtumia Chidi kupata kick

Saturday, 21 May 2016

Babu Tale Alivyoanza Kazi Na Diamond Walifanya Siri, Na Hivi Ndivyo Siri Ilivyovunjika

babu-taleMeneja wa msanii Diamond Hamisi Taletale maarufu kwa jina la Bubu Tale akizungumza na wanafunzi wa Mbezi Beach shule ambayo alisoma na kuwapa ushauri kuhusu kuzifuata njia nzuri za mafanikio na kutimiza malengo katika maisha, aliwapa mfano wa yeye alikopita mpaka kufanikiwa katika mambo yake anayofanya lakini jinsi alivyoanza kufanya kazi na Diamond, Tale alisema kuwa Diamond alimfuata na kumuomba awe meneja wake baada ya kuona kazi aliyokuwa akiifanya, Tale alikubali na kufanya siri kwa mala ya kwanza kwa kuogopa skendo za magazeti kipindi hicho Diamond alikuwa akiandikwa sana katika magazeti. ilikuaje mpaka siri ikavujika na kujulikana kama ni meneja wa Diamond huyu hapa tale akielezea….


                                                   CLICK HAPA KUONA VIDEO
 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes