BREAKING NEWS
Showing posts with label Gigy Money. Show all posts
Showing posts with label Gigy Money. Show all posts

Thursday, 9 June 2016

Naangalia Pesa Kabla Sijamkubali Mwanaume – Gigy Money

 Baby-Madaha
Msanii wa Bongo Fleva na video queen, Gigy Money amesema kuwa anaangalia pesa kabla hajamkubali mwanaume.

Akiongea na Times FM, Gigy Money alisema, “naangalia pesa kabla sijamkubali mwanaume, unajua kuwa na mtu maskini inaleta stress tu, napenda pia wanaume wazuri,” alisema.
Gigy ametokea kupata umaarufu kutokana na maisha yake controversial.

Saturday, 4 June 2016

Lulu DivA na Gigy Money Wapeana Makavu Live

WAUZA nyago kwenye video za Kibongo, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ na Gift Stanford ‘Gigy Money’ hivi karibuni wamechimbana mikwara na kupakana shombo kila mmoja akimuona mwenzake kituko kutokana na maneno anayoyasikia juu yake.

Ishu nzima ilianza baada ya mwandishi wetu kupata ubuyu kutoka kwa mmoja wa watu wa karibu wa Lulu Diva kuwa anamhofia Gigy Money kumfunika katika gemu wanalofanya.

Baada ya mwandishi wetu kupewa ubuyu huo alimwendea hewani Lulu, aliposomewa  madai hayo mwanadada huyo alisema;

“Nani kakwambia hivyo? Siwezi kumhofia Gigy kwenye kile ninachokifanya, hana kitu chochote cha kunifanya nimhofie maana ni mtu wa kawaida sana kwangu.”

Kwa upande wa Gigy alipotafutwa alisema; “Siwezi kupigizana kelele na huyo demu, anatafuta kiki kupitia kwangu lakini hawezi kuipata hata kwa dawa, haniwezi kwa kila kitu, akajipange sana na akae akijua simuogopi.”

Global Publishers

Tuesday, 24 May 2016

Nampenda Matonya Sababu Anajua kuhonga – Gigy Money

Giggy-Money-na-Matonya1-559x520
Akizungumza katika kipindi cha Kubamba cha Times Fm Jumapili, Gigy aliweka wazi mahusiano yake na Matonya ambapo alimpigia simu ‘live’ redioni na kuzungumza kimahaba huku akijinasibu kwa dhati kuwa Matonya ni miongoni mwa wapenzi wake wanaohonga vizuri.
“Nimechoka kuulizwa kila siku juu ya Matonya ngoja nimpigie umsikie mwenyewe(anampigia)” alisema Gigy na kumpigia simu Matonya.
“Unajua nampenda sana Tonya kwa sababu anajua kuhonga aisee, namuelewa sana yani,” alimaliza.

Bongo5

Friday, 20 May 2016

Nay wa Mitego: Gigy Money Anatafuta Kiki Kwangu

MKALI wa Ngoma ya Saka Hela, Emmanuel Elibariki ‘Nay wa Mitego’ ameamua kumfungukia muuza nyago kwenye video za Kibongo, Gift Stanford ‘Gigy Money’ kuwa anatafuta kiki kutumia jina lake katika mahojiano anayofanya na vyombo mbalimbali vya habari.

Akichonga na Showbiz Xtra, Nay alisema kuwa amekuwa akisikia juu ya Gigy akimsema si chochote kwake na kwamba ni mbahili alishawahi kumlipa elfu ishirini baada ya kumaliza kutengeneza video zake.


 “Yaani huyo Gigy anatafuta kiki, namshangaa sana kila sehemu kunisema hovyo, kwanza hatuendani kwa chochote,” alisema Nay.

Hivi karibuni katika mahojiano na Global TV Online, Gigy alisikika akimponda Nay kuwa ni mtu bahili na haitakuja kutokea yupo naye iwe kikazi ama vyovyote kwa kuwa hana hadhi ya kuwa naye.

New AUDIO | Gigy Money Ft. Matonya - SUPU | Download

                                                   DOWNLOAD via HULKSHARE
http://old.hulkshare.com/dl/ap5tg3xdn9c0/Gigy_Money_ft_Matonya_-_Supu.mp3?d=1
 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes