BREAKING NEWS
Showing posts with label Diamond Platnumz. Show all posts
Showing posts with label Diamond Platnumz. Show all posts

Wednesday, 3 August 2016

Download Audio | Chegge Ft Diamond - Acha Waoane

https://my.notjustok.com/track/download/id/116523   Audio |  Chegge Ft Diamond - Acha Waoane| Mp3 Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/116523

Saturday, 23 July 2016

Diamond Platnumz Kwenye Post ya Mtandao wa TIDAL Ya Jay Z...!




post-feature-image
Wiki hii mtanzania Diamond Platnumz amekuwa miongoni mwa wasanii waliofanya show kwenye tamasha la wasanii na muziki wa Afrika la #OneAfricaMusicFest Mjini New York na wakati yupo kwenye show mtandao wa TIDAL Wa kuonyesha muziki uliweka show hio Live na Hii ndio post yao kuhusu Show ya Diamond Platnumz.
tidal 12

Tuesday, 19 July 2016

Jose Chameleone Katika Bifu Zito na Diamond Platnumz....? Ukweli Halisi Huu Hapa

post-feature-image


Msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone amefunguka kwa kusema kuwa hana tatizo na hit maker wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz.

Mitandao ya kijamii ilidai wawili hao hawakuwa sawa kwa muda mrefu kutokana na madai ya kuwa Jose Chameleone kumdengulia Diamond baada ya kuombwa kolabo, lakini hakuna aliyewai kuzungumzia tetesi hizo.

Jumanne hii Jose amesema hakuwai kuwa na tatizo na Diamond kama baadhi ya watu wanavyozungumza.

“I know how much hard work it takes to build a name and how we are all relevant to flying Africa Music to the world. I can see people trying to build beef lines between me and Diamond Platnumz all these years,” aliandika Jose kupitia instagrm.

Aliongeza, “All I can say is go higher my brother the sky ain’t the limit.Stay strong and God bless you more,”

Baada ya kusema hivyo, mashabiki wa Diamond pamoja na wadau mbalimbali wa muziki katika mitandao ya wamempongeza Jose Chameleone.

Friday, 1 July 2016

Diamond Platnumz Aweka Picha Ya Alikiba Kwenye Ofisi Yake, Itazame Hapa...!

Meneja wa Diamond, Babu Tale ameonyesha kuwa wao hawana tatizo na Alikiba baada ya kupost kipande cha video kinachoonyesha picha ya msanii huyo ndani ya studio ya Wasafi Records.
Bongo
Ni muda mrefu imezungumzwa kuwa Diamond na Alikiba wana bifu mpaka kupelekea kuanzishwa kwa baadhi ya team za mitandaoni za kukejeli mafanikio ya msanii wa team nyingine lakini hiyo ni dalili kuwa ipo siku itabaki historia tu.
Babu Tale alipost kipande hicho cha video kinachoonyesha baadhi ya picha za wasanii wakubwa Bongo akiwemo Marehemu Bi Kidude, Mr Blue, Dully Sykes, Juma Nature, Q Chief, Alikiba na wengine wengi.
Je, hiyo inaweza ikawa ndiyo kiki ya kuikaribisha video ya wimbo mpya wa Diamond aliowashirikisha P Square ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni?
Tazama video hapa.

Sunday, 5 June 2016

Diamond Platnumz Afunguka Kuhusu Wema Sepetu

Akiwa kwenye kipindi cha Friday Night Live cha EATV, Diamond Platnuzm amesema kitendo alichofanya Wema kupost kazi zake anadhani imefika wakati labda Wema Sepetu ameona hakuna sababu yeye kuendelea kumchukua Diamond Platnumz na ndiyo maana ameonyesha upendo kwa kusupport kazi zake na za wasanii kutoka kwenye Label yake.


“Kuna wakati inafika watu mnakuwa mmekuwa labda, mtu anaona hana sababu ya kuendelea kukuchukia au kuwa na vita na wewe, sababu mwanzo mwanzo mkiwa bado mnaenda mnaona kuna vitu mko navyo ndiyo maana kuna kuwa na chuki kubwa, lakini ikifika wakati kila mtu amesonga mbele na maisha yake, ameridhika na maisha yake anaona kwanini nimuwekee vita mtu fulani hivyo nadhani labda wakati huo ndiyo huu maana mwenyewe nimeona kweli amepost BET, amepost promo ya Rich Mavoko kwangu mimi nafurahi kwa sababu naona haina faida kwa sisi wasanii kuwekeana vita” alisema Diamond Platnumz

Mbali na hilo Diamond Platnumz alidai toka ameachana na Wema Sepetu hana namba yake ya simu, hajawahi hata siku moja kumpigia simu wala Wema Sepetu hajawahi kumpigia simu Diamond Platnumz.

Diamond Asema ‘WCB’ Imeajiri Watu 42, Azungumzia Issue Ya Kulipa Kodi

Mkali wa muziki na CEO wa label ya WCB, Diamond Platnumz amesema label yake mpaka sasa tayari imeajiri watu 42.
05diamondtuzo5
Muimbaji huyo ambaye pia anamiliki, studio ya picha pamoja na studio ya muziki ‘Wasafi Record’, aliwaambia waandishi wa habari hivi karibuni kuwa kila anachokipata anagawana na team yake.


“Tunashukuru mungu kile tunachokipata tunagawana na wengine, mpaka sasa tayari WCB imeajiri watu 42, hii ni hatua kubwa sana katika tasnia ya muziki wetu,” alisema Diamond.
Katika hatua nyingine, Diamond amesema ni swala la kiungwana kulipa kodi katika kile anachopita.
“Unajua katika kila penye biashara ni lazima na ni haki kulipa kodi ili pato la taifa liingie, namna ya mapato maana yake nini, serikali inatambua kazi na inailinda. So serikali ipo na inafanya hivyo, lakini labda kuna nyanja nyingine hawazioni, kwa hiyo sisi kama tunataka kazi zetu zichangie pato la serikali, lazima tuwe mstari wa mbele katika kuonyesha nyanja zote za mapato, kwamba tunafanya hichi na hichi, ridhiki zetu zinatokea hapa na hapa, mishahara yetu tunagawa hivi na hivi, na kama serikali inavyoagiza katika kiasi hichi tunatakiwa kutoa kiasi hichi kwa ajili ya serikali. Kwa hiyo tusilalamike tu serikali haifanyi kazi wakati sisi tunaweza kuwa wa kwanza kuirahisishia serikali kutekeleza majukumu yake,” alisema Diamond.

Saturday, 4 June 2016

Mambo 5 Tuliyoyaona Baada ya Rich Mavoko Kusainishwa na WCB Wasafi.

Jana ilikuwa siku kubwa kwa label ya WCB inayomilika na Diamond Platnumz. Kwa mara ya kwanza ilifanikiwa kumsainisha msanii mkubwa anayesifika kwa utunzi na uimbaji wa hali ya juu. Kwa kumsajili Rich Mavoko, WCB ilikuwa kama vile timu ya soka inapomsajili mchezaji maarufu na tena kwa dau kubwa.

Mavoko ameungana na Diamond mwenyewe pamoja na wasanii waliosainishwa awali, Harmonize na Raymond. Pia katika utambulisho wa label hiyo ulioendana sambamba na kumtangaza Mavoko kama msanii wake mpya, Queen Darleen, dada yake Diamond naye alitambulishwa rasmi kama sehemu ya roaster ya wasanii wa Wasafi Records.

Haya ni mambo matano ambayo nimeyabaini kwenye hatua hiyo:

1. NI ISHARA NYINGINE KUWA MUZIKI WETU UMEKUA
Pale tasnia ya muziki inapokuwa na record label za uhakika, ni ishara kuwa muziki umekua sana na unazidi kuwa rasmi. WCB wanaelekea kuanza kufanya mambo tuliyokuwa tukiyasikia kwenye nchi zilizoendelea tu. Nigeria ndipo wanapotupigia bao. Wana utitiri wa label zenye uwezo wa kugharamia mambo mengi kwa msanii na akafanikiwa kutengenezwa na kubwa mkubwa.

Utambulisho wa Mavoko uliandaliwa katika ukubwa ambao unaonesha kuwa WCB ipo serious na biashara ya muziki. Ndiyo maana, Katibu Mkuu wa Baraza la Sanaa la Taifa, BASATA, Godfrey Mngereza ameipongeza label hiyo.

“Ni vizuri sana tunapowaona wasanii watanzania wanawekeza katika industry ya muziki, kwa hatua hii inaondoa ile dhana kwamba wanaoweza kuwekeza kwenye muziki ni watu toka nje, kwahiyo ni hatua kubwa sana, ni hatua ya msingi sana ambayo Diamond na timu yake yote wameipiga katika kuonyesha dhahiri kwamba kila kitu kinawezekana,” alisema Mngereza Alhamis hii.

“Huu ni mfano kwamba ameingia hatua nyingine ya kuwa na label. Msanii kuwa na label ni hatua ya juu sana katika industry ya sanaa, kwahiyo kwa vyovyote vile tuweze kumpongeza Diamond, na serikali ipo na inatoa support kwa asilimia mia. Kwa Diamond na mameneja wake, lakini na team nzima ya Diamond, kwamba wanachokifanya, si kwa manufaa yao tu, lakini ni kwa manufaa ya maendeleo ya tasnia nzima ya sanaa na taifa kwa ujumla,” alisisitiza.

2. RICH MAVOKO AMECHUKUA UAMUZI MUHIMU MAISHANI MWAKE
January 29 niliandika makala kuhusu iwapo Rich Mavoko kusainishwa kwenye label ya Wasafi kunaweza kuwa kitu sahihi. Kwa mtazamo wangu, huu ni uamuzi muhimu zaidi ambao Rich Mavoko amewahi kuufanya kwenye maisha yake. Kwa kujiunga na label ya Diamond, hitmaker huyo ni sawa na mmea uliokuwa umeathirika na ukame na kisha kupata matone ya mvua na hivyo kuchipuka zaidi.

Mavoko sasa ana maisha mapya, uhakika zaidi katika muziki kwa kuwa kwenye label ya kwanza kubwa Tanzania inayofanya kazi zake kama label zilizopo kwenye nchi za wenzetu. WCB kupitia Diamond si label yenye wasiwasi wa vitu vidogo tena kama bajeti ya kufanya video nzuri, studio, photoshoot, wapiga picha na vitu vingine ambayo wasanii wengi vinawaumiza kichwa.

Mavoko anarudi tena kwenye chati, kwenye midomo ya watu, mtandaoni na kwenye vyombo vya habari, na muda si mrefu anarejea tena kuwa miongoni mwa wasanii wanaopiga show nyingi zaidi Tanzania. Hilo liko wazi hasa ukiangalia mabadiliko waliyonayo Harmonize na Raymond tangu wawe chini ya label hiyo ambao kwa sasa wana msululu wa show zinazolipa.

Ni kama vile kila anachokigusa Diamond hugeuka kuwa dhahabu. Hakuna shaka tutashuhudia Mavoko akigota vilele ambavyo kama angeamua kujaribu mwenyewe ingekuwa safari ndefu na yenye mitihani mingi.

3. KWA DIAMOND BIASHARA KWANZA, USHINDANI BAADAYE
Unapomuona msanii akichukua vijana wenzake kuwasaidia ilhali akiujua uwezo wao kuwa ni wa kuotea mbali, basi hapo ni wazi kuwa anafikiria biashara zaidi kuliko ushindani. Label ni biashara maarufu sana kwenye muziki – in fact ndicho kiini cha muziki wa Marekani. Kwa wenzetu, ni ndoto kwa msanii kutoka mwenyewe bila kupitia record label na wale waliofanikiwa hivyo ni wa kuwahesababu.

Label nyingi kama Def Jam, Warner Music, Universal Music, Sony Music, Atlantic Records ni makampuni yenye uwekezaji wa mabilioni ya dola za watu ambao hata hawatajwi kwenye vyombo vya habari. Kwahiyo pale ambapo msanii anayeendelea kustruggle kwenye muziki lakini akaamua kuwasaini wasanii wenzake, hahofii tena ushindani. Mawazo ya msanii kama huyu ni ya kiujasiriamali zaidi. Na kwa mkataba wa miaka kumi aliosaini Mavoko WCB, pande zote zitaneemeka na huo ni uwekezaji usio na shaka kabisa.

4. MAVOKO NA DIAMOND WANA CHEMISTRY
Mimi ni mmoja wa watu ambao nimeshangazwa na jinsi Rich Mavoko na Diamond wametengeneza chemistry halisi ndani ya muda mfupi. Sina uhakika, lakini sijawahi kusikia iwapo waliwahi kuwa marafiki huko nyuma. Na nakumbuka kuna wakati kulikuwepona ushindani mkubwa katika ya wawili hawa kiasi ambacho kulizaliwa hadi tension ambayo mara nyingi kwa wasanii wengi zimewahi hata kusababisha uadui.

Na hiyo ndiyo ilikuwa shaka kubwa ya watu wengi tangu tetesi za Mavoko kusainishwa WCB zilipoanza kuvuma. Wengi walikuwa na wasiwasi kuwa fahari huyu ataweza kuwa chini ya fahari mwenzake? Picha na video zinaongea jumbe maelfu kuwa wawili hao wana upendo halisi wao kwa wao na Diamond ni kama mzazi anayejivunia kuwa na Mavoko.

Video aliyoipost Diamond ya sherehe ya kumkaribisha staa huyo WCB ikimuonesha akiimba wimbo Ibaki Story, ni kithibitisho kuwa mastaa hao wana chemistry ya nguvu.

5. MAVOKO ANA FURAHA
Naamini moyo wa Rich Mavoko una furaha kubwa sasa. Hicho ni cha muhimu zaidi kuliko hata matarajio mengine makubwa aliyonayo. Tena, video zinaonesha jinsi alivyofurahia kujiunga na himaya hiyo. Support anayopewa na timu nzima ya WCB sasa ni ishara tosha kuwa yupo kwenye mikono salama.

PICHA: WASAFI CLASSIC INSTAGRAM

Imeandikwa na Fredrick Bundala

Zari ni Mjamzito Tena ? Mama Yake Diamond Amethibitisha Kwa Maneno Haya

Muda si mrefu sana toka Zari na Diamond Platnumz wamepata mtoto wao wa kwanza kwa jina

Kupitia mtandao wa Instagram Mama wa Diamond Platnumz amepost picha ya pamoja akiwa na Diamond Platnumz pamoja na Zari na kuandika "ETI MAMA .K...".


 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes