BREAKING NEWS
Showing posts with label Entertainment. Show all posts
Showing posts with label Entertainment. Show all posts

Monday, 18 July 2016

Mwaimbaji Shaa Hayupo Tena Katika Lebo Hiyo Inayomilikiwa na Master Jay

Malikia wa uswazi kama mwenyewe anavyopenda kujiita Shaa ameweka wazi zile tetesi zilizokuwa zimezagaa kwamba ameondoka Mj Record na kesema ni kweli hayupo chini ya lebo hiyo lakini haimaanishi kwa hafanyi kazi na studio za Mj .

Hata hivyo Shaa amesema ameanzisha kampuni yake inayoitwa SK ambayo ni matokeo ya kazi za sugua gaga,toba na nyingine ambazo zilirudisha gharama za Mj na kumuwezesha kufungua kampuni hake hiyo binafsi ambayo anatarajia kusajili wasanii hata wa tano ila kwa sasa yupo yeye peke yake.

Hata hivyo Shaa ameachia wimbo wake mpya unaoitwa Sawa kupitia kampuni yake hiyo ila unaambiwa Shaa hayupo taari kuyazungumzia mahusiano yake kama ailivyo mpenzi wake Master J ambaye akiulizwa na huwa anajibu lakini kwa Shaa nitofauti kabisaa

Nahreel Alinitengenezea Hit Yangu ya Kwanza Afrika, Siwezi Kuacha Kufanya Naye kazi – Jux

Hivi karibuni kumekuwepo na tetesi kuwa wasanii wengi waliokuwa wakifanya kazi na Nahreel wakiwemo Weusi wameikimbia studio yake ya The Industry baada ya kubadilisha utaratibu wa kurekodi nyimbo.

Jux kwa upande wake amekanusha na kudai kuwa Nahreel bado ni mshkaji wake mkubwa na mwishoni mwa wiki walikuwa pamoja. Anadai kuwa bado ana kazi nyingi kwa producer huyo na kwamba wakati mwingine huamua kubadilisha ladha ili kuogopa nyimbo zake kuzoeleka.

“Nahreel mimi amenitolea hit song, amenitolea ‘Looking For You, naweza kusema ndio wimbo ambao hata Kiafrika ndio ilifanya poa sana,” Jux ameimbia Bongo5.

“Hata kuna wasanii wakubwa wa Kiafrika wengine ambao siwezi kuwasema sasa hivi wameiskia na wameniona huku na tunakuja kufanya nao nyimbo baadaye, ni sababu ya Looking For You. Nisingetoka kwa Bob labda nisingepata kitu tofauti,” amesisitiza.

Kingine amedai kuwa muda wote huu hakuwepo alikuwa nchini China na pia Nahreel amekuwa na miradi yake mingine mingi ikiwemo kwenda Afrika Kusini kufanya video za Navy Kenzo na za wasanii wa The Industry.

“Karudi, tumekutana jana, bado mshkaji wangu na bado nafanya naye kazi pia, sababu ya yeye kubadilisha utaratibu wa studio mimi haijaniathiri chochote kwasababu ni program zake yeye mwenyewe alizotaka kufanya, kwahiyo mimi naona ni sawa. Kwanza mimi ni mmoja wa watu niliyeona hivyo yaani Nahreel alikuwa anadeserve hicho kitu pia kwasababu alikuwa anafanya kazi sana.”

Wiki iliyopita Jux aliachia wimbo wake mpya, Wivu aliorekodi kwenye studio za AM Records.

Bongo5

Wema Sepetu na Idris Sultam Wamwagana Rasmi

DAR ES SALAAM: Ubuyu wa motomoto wa mjini ni kwamba, zile mbwembwe zote za penzi la mastaa wawili Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ na Idris Sultan, zinadaiwa kufikia ukingoni na sasa imebaki stori kwani Wema, Idris wamwagana rasmi.

Wikienda limeng’atwa sikio kuwa, kitendo cha wawili hao ‘kushoo lavu’ kwenye ile Pati ya Black Tie iliyofanyika juzikati katika Ukumbi wa King Solomoni pale Namanga, Dar ilikuwa ni geresha tupu kwani walishamwagana kitambo.

Hata hivyo, kama utakumbuka au hukuipata ni kwamba iliwahi kuvujishwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Wema na Idris wamemwagana lakini baadaye zilivunjwa picha zikiwaonesha wakiwa wameshikana mikono na mahaba tele ili kuua soo.

wema-na-idriss-insta Sasa ubuyu ulionyooka kutoka kwa chanzo cha kuaminika ambacho ni mtu wa karibu wa mastaa hao unadai kwamba, kilichotokea kwenye pati hiyo zilikuwa ni mbwembe za kuzuga zilizotokana na huruma ya Idris.

Ilidaiwa kwamba, Idris alilazimika kufika kwenye sherehe hiyo kwa sababu ilishatangazwa kuwa atakuwa ni miongoni mwa ‘ma-hosti’ lakini ukweli ni kwamba mambo yalishaharibika.

wema na idris 2“Unajua watu wengi hawakujua kuwa Wema na Idris walishaachana kitambo na pale (King Solomoni) walikuwa wanafanya maigizo tu, japokuwa haijulikani moja kwa moja sababu ya kuachana kwao lakini Wema anadaiwa kuwa tatizo kwa Idris kutokana na kutokea kwa migogoro ya kila kukicha,” alitonya sosi huyo.

Hata hivyo, katika kuonesha kwamba kuna kitu kinaendelea, wana-ubuyu wetu walifuatilia akaunti zote za mastaa hao katika mitandao ya kijamii kuona kama mbwembwe zao zinaendelea na kubaini kuwa hawako sawa baada ya kusoma ujumbe wa Wema unaoonesha kumbembeleza Idris huku jamaa huyo akionesha wazi kuwa hakuna mapenzi bali ni drama tu.

Ili kuleta ushahidi, tunakukaribisha hapa kusoma nukuu zao mtandaoni;

MANENO YA WEMA
“Having you as a friend, a brother, a lover and of course a shoulder to cry on every time, i’m at my worst has been the best feeling ever… I wouldn’t want to lose this feeling over anything…
“I realized without u then i ain’t complete…. You have stood by me in good times and bad and even when i messed up so bad you would look me in the eyes and tell me, “Baby, its okay, we gona fix this”…
“Idris you have been one of a kind and losing u is the last thing i want on this earth… I will love you until forever, until death do us part we will be together…
“I will hold on to you till da last minute because together we will get there…. I love you with my life…. For I believe you are my true love, my baby and inshallah! The Man that my kids will call daddy…” alimalizia kuandika Wema akimlilia Idris.

IDRIS NAYE ALIANDIKA:
“Kumbuka kurekebisha kiatu kila hatua ya maisha unayopiga kisije kuchomoka ukakanyaga mwiba ukapunguza spidi.”

WEMA ASAKWA
Wikienda halikuishia hapo kwani lilimsaka Wema anayedaiwa kubwagwa, alipopigiwa simu hakupokea, akaandikiwa ujumbe mfupi wa sms ambao pia hakuujibu.
Pia alitumiwa ujumbe kwa njia ya WhatsApp lakini pia hakujibu.

 UBUYU WAKAMILIKA KWA IDRIS MWENYEWE
Wikienda liligeuza dira yake na kuielekeza kwa Idris ambaye alifunguka bila kuacha lolote.
Kwa mujibu wa Idris, yeye na Wema walishasahau kuwa waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kwani kwa sasa kila mtu ana ‘biashara’ zake.

“Mimi nilikwenda kwenye ile pati kwa sababu ya kuwaonea huruma tu kwani ndiyo kwanza wameanzisha kampuni na mbaya zaidi walikuwa wakiniweka kwenye matangazo. Unadhani watu wangewachukuliaje? Sikutaka kuwaharibia shoo lakini mimi nilishaachana naye na nina biashara zangu nyingine,” alifunguka Idris.

Idris alienda mbali zaidi na kusema kuwa kwa sasa ana mwanamke mwingine anayempenda na siku si nyingi mambo yakikaa sawa, atamuanika.
“Mwenzenu nina kifaa kingine soon nitawafahamisha,” alisema Idris.

WEMA NA IDRIS
Awali Wema na Idris walificha uhusiano wao lakini baadaye waliamua kujiachia ambapo mlimbwende huyo alidai kushika ujauzito lakini kwa bahati mbaya ukachoropoka.

Source:Global Publishers

Huu ndiyo ukweli kuhusu ndoa ya siri ya D’Banj

D’Banj bado hajafunga ndoa ila amemtambulisha mchumba wake kwa wazazi wake na familia yake pekee – kwa mujibu wa chanzo cha habari.

Mapema mwezi huu zilienea taarifa kuwa staa huyo wa muziki kutoka Nigeria, amefunga ndoa na msichana anayedaiwa kuwa na asili ya Afrika Kusini na Nigeria lakini makazi yake ni nchini Marekani, Didi Kilgrow.
Akiongea na Sunday Scoop mtu wa karibu wa D’Banj amesema, “Dbanj has given so much information about himself to the public and he deserves to keep some things private and this is one of those things.”
“He is not worried about losing female fans, he just wants his marriage and the impending white wedding off public radar,” ameongeza mtu huyo.

Kajala Achefua Watu Baada Ya Kuvaa Nguo Inayoonyesha Matiti Yake

KAJ


Kajala Masanja; Bongo Movie Actres Kajala Masanja looks faboulous on new photos of the day

Tuesday, 5 July 2016

Alikiba Afungua Brand Yake Ya Nguo...!

Ali Kiba ameamua kuja na Brand yake ya kofia za AK alikiba kwa ajili ya mashabiki zake na watu wake wa karibu.
Ak(alikiba)👑 New brand cap available..30k
For more information check:0654 367910 or 0652 988888

Monday, 4 July 2016

Darasa Afunguka Kuhusu Ishu ya Linah Kutamani Kuwa Naye, Adai ‘Nina Mpenzi’


Mkali wa Hip Hop Bongo, Sharif Thabiti Ramadhani ‘Darasa’ amefunguka kuwa anaheshimu maneno ya msanii mwenzake, Estalina Sanga ‘Linah’ kuwa anamkubali na kutamani kuwa na mwanaume mwenye sifa kama zake lakini yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu.
Akizungumza na Wikienda alipotembelea Global TV Online wikiendi iliyopita, Darasa alisema kuwa Linah ametumia ujasiri kutoa hisia zake na amefurahi kusikia anamkubali ingawa yeye ana mpenzi wake wa muda mrefu na wanaaminiana.
“Namshukuru kwa kunikubali, kiukweli namheshimu na nimefurahi,” alisema Darasa.
Darasa alifunguka hayo baada ya hivi karibuni Linah kueleza hisia zake kwenye mitandao ya kijamii kuwa anatamani awe na mwanaume mwenye sifa alizonazo Darasa.
Share na Marafiki:

Saturday, 2 July 2016

Wema Sepetu ‘Mimi Dhahabu Inayogombewa na Watu, Sijali Wanaonichafua’


WemaSepetu

Mrembo wa filamu Tanzania, Wema Sepetu, amesema yeye ni dhahabu inayogombewa na watu hivyo hajali hata kama atachafuliwa namna gani katika mitandao ya kijamii.
Wema aliliambia MTANZANIA kwamba, hana mpango wa kujibu vibaya vinavyoongelewa kuhusu yeye kwa kuwa yeye bado ni dhahabu inayotamaniwa kushikwa na kila mtu.
“Mimi ni kama dhahabu hivyo kila mtu anatamani kuishika, watu wanaacha kufanya yao kila siku Wema, kwa sasa niko na mambo yangu ya kutafuta fedha sina habari na mtu hata aniandike vibaya vipi,” alisema Wema.
Aliongeza kwamba licha ya kusemwa, amezidi kujiongezea mashabiki na mikataba mbalimbali ya kufanya kazi na makampuni yenye majina makubwa kwa kuwa yeye ni kama dhahabu isiyochafuka.

Share na Marafiki: 
 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes