BREAKING NEWS
Showing posts with label Harmonize. Show all posts
Showing posts with label Harmonize. Show all posts

Tuesday, 5 July 2016

Audio | Harmonize – Matatizo | Mp3 Download

Nyingine Mpya Toka Kwa Harmonize WCB.. Ngoma inaitwa MATATIZO.. Kuwa Mjanja mtu wangu.. Kuwa wa kwanza kuisikiliza na kuipakua hapa hapa
mp3

Harmonize (Official Video) – Matatizo | Mp4 Download

matatizo videoBaada ya kuisubiri sana video ya Diamond Platnumz akiwashirikisha P Square, WCB wameamua kuachia video mpya ya Harmonize, video inaitwa Matatizo, Sikiliza na kuipakua hapa chini                                                    DOWNLOAD

Monday, 6 June 2016

Harmonize Amnunulia Wolper Gauni La Tsh Milioni 1

IMEVUJA ! ‘Kinda’ wa Bongo Fleva Rajab Abdulhan ‘Harmonize’ ambaye anatamba na kibao chake cha Bado, anadaiwa kumnunulia mpenzi wake, staa wa filamu, Jacqueline Walper ‘Wolper’ gauni lenye thamani ya shilingi milioni moja.
Chanzo kilicho karibu na msanii huyo wa lebo ya WCB, kinadai muigizaji huyo ni mwanamke wa gharama, ambaye mavazi na maisha yake, yanahitaji mtu mwenye uwezo kifedha, lakini kwa kijana huyo mwenyeji wa Mtwara ni kama anajiumiza.
“Yaani hivi karibuni wakati akienda kumtambulisha kwao, alilazimika kumnunulia gauni la shilingi milioni moja wakati yeye mwenyewe anavaa mavazi ya kawaida tu kama wasanii wenzake, hapa kweli mapenzi yamekubali,” kilisema chanzo hicho, kilichoomba hifadhi ya jina lake.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, paparazi wetu alimtafuta Wolper na kumsomea tuhuma hizo, lakini alicheka na kudai hana la kusema kwa vile maisha ya kimapenzi na msanii huyo ni ya kawaida tu.
Harmonize mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, alisema kwa wakati huo hakuwa katika eneo zuri, akiahidi kupiga yeye mwenyewe kwa gazeti hili baadaye lakini hadi linakwenda mitamboni, hakuwa amepiga.
Kwa upande wa meneja wa msanii huyo, Mohamed Salum ‘Rikadomomo’ alisema anamsimamia kimuziki tu, maisha yake binafsi hayamhusu.
-GPL

Monday, 30 May 2016

Maneno Ya kumkejeli Wema Sepetu Yamtokea Puani Harmonize


Harmonize amelazimika kuamka na hangover ya matusi kutoka kwa mashabiki wa Wema Sepetu baada ya kusambaa video inayomuonesha akiwa na washkaji zake akishuka mistari ya hip hop inayoishia kumkejeli ex wa bosi wake, Sepetunga.
HARM
“Nasikiaga uzuri wa nyumba usikufanye utembee peku, sista duu usitoe mimba kesho ulie kama Wema Sepetu,” anaonekana Harmonize akirap na kushangiliwa na washkaji zake. Video hiyo imesababisha hasira kubwa kwa mashabiki wa Wema waliomporomoshea matusi usiku kucha kuanzia jana.
Wema aliupata ujumbe huo na aliamua kuujibu kwa busara zaidi kwa kuweka nukuu ya Angelina Jolie kwenye picha hiyo chini na kuandika tu: Well. Arent you??”
13151360_1072023689554363_894032107_n
Mpenzi wake Idris alijibu pia lakini kama kawaida kwa utani mwingi.
“As i sit here nikakumbuka kitu “Jamani nimeanzisha format yenye ustaarabu na taratibu, kwa yoyote anayetamani kutafuta kiki kupitia mimi kuna contract nimeandaa ni makubaliano mimi na wewe kwa percent ya mapato utakayopata kwa kiki hiyo ili itunufaishe wote tena ntakupa hadi na idea za jinsi ya kunitukana na kunimaliza kwasababu najua mwisho wa siku tunavuta mpunga wetu wanashangaa kesho mi na wewe tunacheka tu” hii naiita #MoneyKick #KikiPesa clients wote email me bei ni maelewano,” aliandika.
Katika kujaribu kuliua soo, Harmonize alijirekodi voice note na kuituma kwa makundi ya WhatsApp ya WCB lakini snitch mmoja aliivujisha na kuiweka Instagram. Kwenye sauti hiyo Harmonize anasikika anasema kuwa siku wanarekodi video hiyo aliomba isisambae kwakuwa aliamini ingekuja kumletea matatizo.
“Bahati mbaya imetokea hatujui nani amevujisha video imeleak,” anasema. Anadai kuwa mkakati waliojadili kufanya ni kuipigia promo ngoma mpya ya Raymond ‘Natafuta Kiki’ ili kumaliza nguvu ya video hiyo.
Kitu anachotakiwa kukifahamu Harmonize sasa ni kuwa kile kinachojadiliwa kwenye magroup ya WhatsApp ya WCB hakibaki humo tu, kuna snitches kibao wanaoweza kuumwaga mchele kwa ndege wengi hasa wasiohusika!

Tuesday, 24 May 2016

Harmonize Atoa Maneno Ya Kejeli Kwa Wema Sepetu, Bifu Zito Latabiriwa..... Angalia Video Nzima Hapa....

 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes