BREAKING NEWS

Sunday, 12 June 2016

Huu Ndio Mwongozo Wa Adhabu Wanazotoa WCB Kama Msanii Wao Akifanya Makosa


Uongozi wa label ya ‘WCB’ umesema umejipanga kikamilifu kudhibiti swala la nidhamu kwa wasanii wake.
13267534_539419969516292_1584784009_n
Akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni, mmoja kati ya viongozi wa juu wa label hiyo, Babu Tale amesema wao kama uongozi watasimama kidete kuhakikisha wasanii wa WCB wanakuwa mfano wa kuigwa kwa jamii.
“Nikijibu hapo kwenye eneo la nidhamu ni kwamba, sisi ni vijana ambao tunaishi na vinaja ambao wametoka kwenye familia zao ambazo zinamalezi tofauti tofauti, lakini wakija hapa ni lazima wafuate sheria zetu. Sitaki kumsifia Dioamond ni mtu ambaye hana nidhamu ya kuigiza, kwa hiyo hawa wengine lazima wafuate tabia za kaka yao,” alisema Babu Tale.
Aliongeza, “Kwetu msanii akitukana kwenye social network , akitukana kwenye stage huyo lazima sisi tumuadhibu. Kuna adhabu ambayo inasukumwa na social network hiyo hatuizingatii kwa sababu kila mmoja ana mapenzi yake na wengine wanachuki zao. Adhabu ambayo tatizo linaonekana wazi kwamba hili ni tatizo, tunayaita matendo kusudi, kiofisi huwenda mtu akasimamishwa bila jamii kujua, kukata pesa kwenye kazi zake bila jamii kujua, hayo mambo tunafanyia hata sisi viongozi pale tunapokosea,”

Nuh Mziwanda Kufanya Bonge La Kolabo Na Tekno Soon...!

Mziwanda-2452524_n

Nuh Mziwanda amesema anakaribia kukamilisha collabo yake na msanii wa Nigeria, Tekno.
Mziwanda-2452524_n
Wimbo wa Jike Shupa ni moja kati ya nyimbo ambazo zinafanya vizuri kwenye redio kutokana na ujumbe uliokuwa ndani yake kumgusa moja kwa moja huku video yake akiwa ameachia jana.
Akiongea kwenye kipindi cha Ala za Roho, kinachoruka kupitia Clouds FM, Nuh Mziwanda alisema, “Tumeshaanza kuongea na Tekno.”
“Jamaa ana uwezo mkubwa, anajua muziki, najisikia faraja kufanya naye kazi. Ni producer mkubwa kama mimi, ni msanii mkubwa mwenye kipaji na tunashabiana maana ni mkali wa melody na wote tunategemea melody,” aliongeza.

Friday, 10 June 2016

Download Audio | Best Nasso - Ukweli Uko Wapi

                              Audio |  Best Nasso - Ukweli Uko Wapi| Mp3 Download


https://my.notjustok.com/track/download/id/99779

Download Video: Best Nasso - Ukweli Uko Wapi?

Thursday, 9 June 2016

Naangalia Pesa Kabla Sijamkubali Mwanaume – Gigy Money

 Baby-Madaha
Msanii wa Bongo Fleva na video queen, Gigy Money amesema kuwa anaangalia pesa kabla hajamkubali mwanaume.

Akiongea na Times FM, Gigy Money alisema, “naangalia pesa kabla sijamkubali mwanaume, unajua kuwa na mtu maskini inaleta stress tu, napenda pia wanaume wazuri,” alisema.
Gigy ametokea kupata umaarufu kutokana na maisha yake controversial.

Raymond wa WCB Wasafi Aringishia Mabunda ya Pesa Mtandaoni, Jionee Hapa


Wakati mtaani raia wakilalamika kuhusu ukata wa hela toka Rais Magufuli aingie madarakani, mkali wa wimbo ‘Kwetu’ kutoka WCB, Raymond ‘Rayvanny’ ameamua kuringisha mabunda ya hela kupitia ukurasa wake wa instagram.
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Natafuta kiki’ amepost picha kupitia instagram yake na kuandika jina la wimbo wake huyo, huku mashabiki wakitoa maoni yao juu ya wingi pesa hizo.

Raymond alisaini ‘WCB’ mapema mwaka huu kabla ya hapo alikuwa anafanya kazi Tip Top Connection huku akiwa karibu zaidi na Madee.

Haya ni maoni ya mashabiki hao.

Tajibetese
Mmmmh @rayvannyy kama unatupenda fans wako hii ndo number yangu 0768046197 hata alfu kumi tuisogeze ramadhan

Blackgal_ake_dede
Hiyo kiki ndio yenyewe sio ya mademu fanya kunigawia basi ndugu @rayvanny

Am_coco_
That’s why I love you ,… Harmo abaki tu kwa mchaga, mi mpare nakutaka wewe .

Celinn1988
Watu wanavyojua kupangia watu kweny hela zao, mtadhani zenu mmefanyia kitu cha maana au mnaropoka tuu hapa.

Wednesday, 8 June 2016

Wolper na Nisha wazinguana kisa Harmonize? Nisha kajiweka kwa Raymond?


Wolper
Drama za mastaa wa bongo movies hazeshi (no typo). Jacqueline Wolper na Salma Jabu maarufu kama Nisha wamepishana lugha huku Harmonize akiwa chanzo.
Wolper
Issue ilianza vingine kabisa. Nisha alipost picha inayowaonesha Ben Pol, Raymond, Nuh Mziwanda na Rich Mavoko na kuandika: Mmoja kati ya hawa amejaa kwenye galary ya simu yangu na moyoni mwangu,otea A B C AU D? enhe. he sa hv siweki hadharani maana nna phd ya kunyakuliwa, sa hivi ni kumpost kwa mwendo kasiii yaani wengi wengi simtaji ng’ooo.
Watu walicheka, walifurahi na kucomment hadi pale comment ya mwana bongo movie mwenzake, Jacqueline Wolper ilipobadilisha kabisa hali ya hewa.
13413370_190305564700163_1704982609_n
13413370_190305564700163_1704982609_n
Nisha alilazimika kuitolea ufafanuzi comment ya Wolper na ndipo mambo yaliyopo nyuma ya pazia yakawekwa hadharani. Seems like Nisha aliandaa show Mtwara na kumchukua Harmonize hali iliyomfanya Wolper naye aende Mtwara – of course kulinda chake kisijekupokonywa!
“Ok guys kuna picture niliweka saa 4 asbh leo,za wasanii kadhaa wa music ambao niliweka na caption yangu kwa furaha zangu tu,” aliandika Nisha kwenye post nyingine.
“Ila baada ya lisaa limoja ikaja coment hiyo ya msanii mwenzangu sikudhungumza chchte,i was like ok nikacheka tu. Then zikaja comments nyingi za kumuuliza kulikoni kuandika hivyo. Masaa mawili yaliyopita ukaandikwa waraka mzito mrefu unaosema. “Nisha aandaa show Mtwara ya kumnasa Harmonize ila Wolper akagundua hilo akaamua kuongozana naye Harmo hadi huko kukwepa hilo (NA MANENO MENGI YA ZIADA YA UONGO.”
“Ikimbukwe show imeshapita km week na haya maneno yamezuka leo baada ya hiyo comment. Guyz tuje kwenye point KWANZA KABISA SIJAMLENGA YYTE KWA NILIYEANDIKA NILIANDIKA KWA MAPENZI YNG KM NILIVYOANDIKA JANA STATUS YA VIDONDA VYA TUMBO,TENA HADI WADOGO ZNG NIKAWAAMBIA TAZAMA NACHEZA NA AKILI ZA WATU. NIMESHANGAA HABARI ZA UONGO KUSAMBAZWA ZIDI YANGU TENA BAADA YA COMENT HII KWANGU,” aliongeza.
“POINT YA PILI KWA YYTE ANAYEULIZA NIMEANZA LINI UPROMOTA guyz mimi ni mfanyabiashara na kwenye pesa nipo,show ya MTWARA imenigharimu si chini ya ml.18 unadhani naweza poteza pesa zote hizo kisa mapenzi?sina ujinga huo wa akili. NA SIJAWAHI KUMTAKA NA SITOTARAJI KWANZA SIJAZOEA KUPITA ANAPOPITA MTU HASWA NNAYEMJUA.”
“TATU nimeandaa show ingine ramadhan ya 13 DAR-ES-SALAAM inahusu ramadhan, nna SHOW SKUKUU YA IDD MOSS NA IDD PILI MIKOANI ZOTE MM NDO MUANDAAJI NA KUNA WASANII WAKUBWA TU JE HAO PIA NATAKA KUWANASA? HE. IFIKE HATUA TUSIWE TUNABALANCE MTU MMOJA NA PIA SIO KILA ASIYEDHUNGUMZA NI MNYONGE SANA ILA KUNA WKT DRAMA HAZINA MUDA INABIDI UPIGE KAZI MAANA MAISHA YANAENDA MBELE HAYARUDI NYUMA. NB:SHUKRAN KWA WEWE UNAYESAMBAZA UJUMBE HUU WA UONGO SINA CHA KUKWAMBIA NIMEPITIA MENGI MAKUBWA SO HILI KM NACHEZA MDAKO. (mwenye uelewa kaelewa chanzo cha story inayosambaa imetoka wapi,nimeandika hapa kwa manufaa ya mashabiki zangu wote watakaobahatika kusoma habari hizo za uongo.”
Na sasa hebu turejee kwenye post ya mwanzo kabisa ya Nisha. Ni msanii gani kati yao hao wanne ambaye yupo moyo mwake kwa mujibu wa maneno yake mwenyewe? Tuanze kudadafua:
BEN POL
Hapana, juzi tu ametoka kuwa baba na mwanae anaitwa Mali aliyezaa na mchumba wake wa muda sasa Latifa Mohamed. Jamaa ni mwaminifu.
NUH MZIWANDA
Hapana, juzi tu ameanza kumuonesha mpenzi wake ambaye tayari amejichora tattoo yake. Sio rahisi!
RICH MAVOKO
Hapana, juzi tu mwanae amefikisha siku 40 na kumtoa nje kwa mara ya kwanza na Diamond alikuwepo. Ni ngumu.
RAYMOND
Ewalaaah.. tunaweza kumfikiria hitmaker huyu wa Kwetu kwasababu hadi sasa hajamweka hadharani mpenzi wake.
Ifahamika tu kama alivyosema Nay wa Mitego.

Bongo5

 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes