BREAKING NEWS
Showing posts with label Udaku. Show all posts
Showing posts with label Udaku. Show all posts

Tuesday, 19 July 2016

Mtoto wangu wa kike ataitwa Karma – Wema


wema

Malkia wa filamu Wema Sepetu bado hajakata tamaa kuhusu kupata mtoto licha ya kukatishwa tamaa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii kutokana na uzazi wake kuwa mgumu.

Muigizaji huyo ambaye alianzisha mfumo wa APP na SMS ambao unatoa taarifa zake mbalimbali kwa mashabiki juu ya maisha yake, tayari umeanza kutoa taarifa mbalimbali kuhusu maisha yake.
Kupitia mfumo huo, Wema amesema angependa mwanae wakiume ampatie jina la Karma.
“Mtoto wangu wa kiume ataitwa Karma,” alisema Wema. “Bado sijafikiria jina nitakalo mpa mtoto wangu wa kiume japo namtaka sana mtoto wa kwanza awe wa kiume, Mungu anajua,” alisema Wema.
Pia kupitia system hiyo, Wema amewashukuru mastaa wenzake wa filamu ambao walimsupport katika show yake ya ‘The Black Tie’.

Jose Chameleone Katika Bifu Zito na Diamond Platnumz....? Ukweli Halisi Huu Hapa

post-feature-image


Msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Uganda, Jose Chameleone amefunguka kwa kusema kuwa hana tatizo na hit maker wa wimbo ‘Kidogo’, Diamond Platnumz.

Mitandao ya kijamii ilidai wawili hao hawakuwa sawa kwa muda mrefu kutokana na madai ya kuwa Jose Chameleone kumdengulia Diamond baada ya kuombwa kolabo, lakini hakuna aliyewai kuzungumzia tetesi hizo.

Jumanne hii Jose amesema hakuwai kuwa na tatizo na Diamond kama baadhi ya watu wanavyozungumza.

“I know how much hard work it takes to build a name and how we are all relevant to flying Africa Music to the world. I can see people trying to build beef lines between me and Diamond Platnumz all these years,” aliandika Jose kupitia instagrm.

Aliongeza, “All I can say is go higher my brother the sky ain’t the limit.Stay strong and God bless you more,”

Baada ya kusema hivyo, mashabiki wa Diamond pamoja na wadau mbalimbali wa muziki katika mitandao ya wamempongeza Jose Chameleone.

Sunday, 10 July 2016

Kiki za Mastaa Zilizotingisha, Shilole, Vanessa Mdee, Ray Kigosi, Rubby, Aslay….

KIKI siyo kitu kigeni kabisa kwa wasanii ulimwenguni. Kutafuta jambo la kushtua na kuwafanya mashabiki wamzungumzie msanii husika kwa muda mrefu zaidi akiwa na lengo la kuachia kazi yake.


Lakini kwa baadhi ya wasanii wetu hapa Bongo hujiingiza kwenye skendo wakidhani ni kiki. Kwa kawaida kiki ni nzuri ili kumsaidia msanii kujipaisha na kuchomoa kazi yake, lakini si kwa kujiharibia kwa kashfa mbaya ambazo mwisho wake kufutika inakuwa shida.

Yes! Hapa Bongo wapo mastaa wengi ambao wametingisha kwa kiki huku wengine wakijaribujaribu. Polisi wa Swaggaz anakudondoshea kiki za mastaa zilizotingisha zaidi tangu kuanza kwa mwaka huu.

RUBY, ASLAY

Kila mtu aliongea lake ilipovuma kuwa Ruby anatoka na Aslay ambaye kiumri ni mdogo kwake. Hii ilitokea Juni 13, mwaka huu mara baada ya Ruby kuanza kutupia picha za Aslay kwa fujo kwenye ukurasa wake wa Instagram na kuandika meneno yanayoashiria kuna mahaba mazito kati yao.

Aslay yeye alimjibu Ruby kwa jumbe tamu za mahaba na kuzidi kuwachanganya mashabiki huku wengi wakitamani kuona kama penzi hilo jipya mjini litakuwa na uzito wa kuipiku kapo ya Harmonize na Wolper iliyokuwa inatamba kipindi hicho.

Wakati watu wengi wanazidi kumiminika na kuifuatilia kapo hii ndipo Yamoto Band wakaachia ngoma yao mpya inayoitwa Suu, waliyomshirikisha Ruby.

Ikasanuka kumbe ilikuwa kiki tu. Hilo lilithibitishwa hata na meneja wao Said Fella ‘Mkubwa Fella’ a.k.a Mheshimiwa Diwani.

LINEX

“Ahsante Mungu, kuna maamuzi hayahitaji matangazo, silence speaks  volumes,” aliandika Linex kwenye ukurasa wake wa Instagram mara baada ya kutupia picha akiwa kwenye mikao tofauti na mrembo aliyedai kuwa amemuoa.

Linex alizidi kupokea pongezi kutoka kwa mashabiki waliovutiwa na tukio la yeye kufunga ndoa, uamuzi ambao ni nadra mno kwa wasanii wa Bongo Fleva.

Hali ilikuwa tofauti mara baada ya kutumia picha zilezile za harusi kutengeneza kava la ngoma yake mpya iitwayo Kwa Hela, aliyoachia mwanzoni mwa mwaka huu.

Kwa tukio hilo, Linex alijikuta akipokea matusi kutoka kwa mashabiki kwa kosa la kuchezea hisia zao lakini mbali na kadhia hiyo lengo lake la kutumia Kiki lilifanikiwa, aliapoachia ngoma yake ikapenya.

RAY KIGOSI

Vincent Kigosi ‘Ray’ alifanikiwa kuwakamata mashabiki wake kwa kutengeneza kiki yenye ‘akili’ sana. Yeye aliibuka na maelezo kuwa weupe wake ni kwa sababu anatumia maji mengi na kushiriki mazoezi.

Ray alisema hayo wakati akihojiwa na kituo kimoja cha runinga jijini Dar es Saalam. Hakuna kiki inayofikia hii tangu mwaka huu umeanza. Katika mitandano ya kijamii watu mbalimbali walipiga picha wakiwa wanakunywa wakidai wanataka kuwa weupe kama Ray!

Ile kushangaashangaa, Ray akaachia Filamu ya Tajiri Mfupi ambayo ilifanya vizuri sokoni. Pamoja na kiki hiyo, Tajiri Mfupi ni kati ya sinema bora za Kibongo zilizotoka mwaka huu.

VANESSA MDEE

“Nikupe Kiki ujulikane au siyo? Kila siku twanyamaza ndiyo mtugaragaze. Mimi siyo wale uliowazoea,” aliandika Vanessa Mdee kwenye instagram akimshambulia Shilole.

Shilole hakukaa kimya naye kupitia ukurasa wake wa Instagram aliandika: “Veepe jipange sana, mwenzio Igunga niliaga, sijaletwa kwa kubebwa kwenye lori, nimekuja na mbio za mwenge. We si wa magorofani na kiingereza chako cha kuunga mi ndo mtoto wa mbwa, sasa ole wako tukutane utanyooka.”

Watu wakahamishia mawazo yao kwao, kutahamaki kumbe walikuwa wanaandaa shoo Club Bilicanas, Dar. Shoo ilikuwa poa kutokana na kiki hiyo.

NEDY MUSIC

Baada ya Shilole kumwagana na Nuh Mziwanda watu walikuwa wanatamani kufahamu ni nani ataziba pengo hilo. Ghafla kijana mdogo Nedy Music akaanza kuhisiwa kutoka kimapenzi na mwanadada huyo.

Sababu kubwa iliyofanya watu waanze kuhisi kuwa kuna penzi kati yao ni picha walizokuwa wanatupia kwenye Instagram zikiambatana na maneno ya mapenzi.

Hakuna aliyemjua Nedy Music kabla ya kuwa na Shilole lakini alipata umaarufu mara baada ya kiki hiyo ya kumrithi Nuh Mziwanda, hata  alipoachia ngoma yake Usiende Mbali chini ya Ommy Dimpoz kupitia lebo ya PKP alichomoka kirahisi tu.

Na hapo ndipo ikajulikana kuwa hakukuwa na mapenzi kati yao bali ilikuwa kiki ya kutafuta mashabiki kwenye muziki huu wenye ushindani. Kwa hilo alifanikiwa.

Diamond na Zari Waweka Video yao Wakiwa Nusu Utupu Baada ya Kumaliza Mechi Sita Kwa Sita..Tazama Hapa

Instagram inazidi kuwa sehemu ya mastaa kujitamba na mambo tofauti wanayofanya kwenye maisha yao kama vitu vya kifahari, mali zao na watoto wakali wanaotoka nai,

HAMISA Mobeto Afunguka Tuhuma za Kutoka na Diamond Kimapenzi Zilizoenea Mtandaoni


Hamisa Amefunguka haya baada ya tetesi kuzagaa mtandaoni kuwa yeye ndio chombo kipya cha Diamond baaada ya kuonesha ukaribu zaidi na familia ya Dai:

"Eti Mdau anauliza kama ilikuwa kazi mbona hukupiga picha na Madam Zari?
Chaaaa!!! From @hamisamobetto - Binadaamu banaa.......
Now days U cant work with anyone wala kua close na yoyote just because unaogopa maneno yatakayo zuka after hiyo shughuli ...
@kendrah_michael @_esmaplatnumz
A birthday to remember 2016
#MamasBigDay ....... Na nshaanza kupokea emails za kazi ety...haya kama unataka upendezeshwe na Hamisa mobeto ung'are sherehe yako iwee ya kuvutia kindly contact me kwa email ya apo kwenye Bio
#HapaKaziTu ...Cc the boss @diamondplatnumz"

Tuesday, 5 July 2016

Moses Iyobo Amtaka Mama Cookie Ajichore Tattoo Kama Shilole

Dansa kutoka Wasafi Classic Baby (WCB), Moses Iyobo ‘Moze’ ambaye ni mzazi mwenza wa staa wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel Grayson, amemwambia mpenzi wake huyo kuwa na yeye ajichore ‘tatuu’ ya jina lake kama ilivyokuwa kwa msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kwa Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kabla ya kumwagana.

Moze alimwambia hayo Aunt baada ya mwanadada huyo kujichora mkononi kwa kalamu maneno yaliyosomeka; ‘Aunt wa Mose Iyobo’ ambapo jamaa huyo alimsisitizia kuwa kama kweli anamaanisha hivyo, basi ajichore kama Shilole alivyofanya kwa Nuh.

“Kama mama Cookie (mtoto wao) anataka kujilipua, ajichore kama Shilole alivyofanya kwa Nuh maana alivyojichora kwa kalamu, hata akioga, inatoka,” alifunguka Moses.

Monday, 4 July 2016

​Picha: Ommy Dimpoz, Wayne Rooney Wakila Bata Ibiza, Hispania

Kama kuna sehemu inayotembelewa zaidi duniani na watu ambao hawana kabisa stress ya kitu kinachoitwa ‘Pesa’ basi Ibiza, Hispania inaongoza.

Ibiza ni kisiwa cha raha, burudani, starehe na bata la kila aina. Ni sehemu ambayo nyota wa Manchester United na England, Wayne Rooney na familia yake wanapumzika kwa sasa baada ya timu yake ya taifa kutolewa kwenye Euro 2016.
Ommy Dimpoz ni miongoni mwa watu wanaofurahia hewa ya Ibiza kwa sasa.

Hitmaker huyo yupo kisiwani humo katika kile kinachoweza kuwa ni ‘vekesheni’ yake ya aghali zaidi kuwahi kuifanya.

Anamfanya kila mtu aone wivu kwa maisha na raha anayopitia sasa. Kucruise kwenye speed bot na kuchezea maji ya bahari ya Mediterranean.

Staa huyo amepost video akiwa kwenye boti na watu wengine wawili, msichana , Milly na nahodha wa kizungu aliye kifua wazi. Hakika Ommy katisha.

Barakah Da Prince adai hajawahi kuupenda muziki wa Young Killer

Msanii wa muziki, Barakah Da Prince, amefunguka na kusema kuwa yeye si shabiki na wala hapendi muziki anaoufanya rapa na mzaliwa mwenzie wa Mwanza Young Killer Msodoki.Barakah Da Prince
Muimbaji huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Siwezi’ ameiambia Times Fm, kuwa hapendi muziki wala hajawahi kupenda kazi yoyote ya Msodoki.
“Sijawahi kupenda muziki anaoufanya Killer,” alisema Barakah. “Mi sio shabiki yake kabisa, najua ndio anatokea home na nini lakini sipendi muziki wake,”
Katika hatua nyingine amesema rapa anayemkubali zaidi ni Young Dee kwa kuwa anauwezo wa kubadilika kulingana na Mazingira.

Bongo5.com

 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes