BREAKING NEWS

Wednesday, 8 June 2016

Jionee Video ya Sanamu La Freemason iliyopo Nyumbani Kwa Nay wa Mitego


Wa mitego amekua akihusishwa sana na Freemason, hii ishu haijaanza leo imeanza toka kitambo. Hii ni kuanzia alama ambazo mara nyingi amekua akizionyesha katika video zake na hata namba za gari zake 3 ambazo zimekua zikihusishwa na mambo ya Freemason.

Sasa Nay Wa Mitego kaamua kutuonyesha na sanamu iliyo sebuleni kwake ambayo bila ubishi ni sanamu ambayo hutumika kuwatambulisha Freemason. Katika video hiyo ameonekana Nay akiwa na mtoto wao huku sanamu hiyo ikiwa kama moja ya pambo sebuleni hapo. Jioneee video hiyo hapa chini... 

"Kuna Msanii Mkubwa Hakupenda Mimi Kujiunga na WCB" – Rich Mavoko

Msanii mpya kutoka lebo ya WCB, Rich Mavoko amesema kuna msanii mkubwa bongo alimkataza kujiunga na WCB.

Akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo, kinachoruka kupitia EA Radio, Rich Mavoko amesema kuna msanii mkubwa alimtumia ujumbe wa simu na kumuuliza kwanini amekubali kwenda kusimamiwa na Diamond.

Sijawahi kusema hili ila ukweli ni kwamba wakati nataka kwenda WCB kuna msanii mkubwa alinitumia ujumbe na kuniambia Rich Mavoko unakwendaje kusimamiwa kazi zako na Diamond Platnumz, kiukweli aliniumiza sana ila nilimjibu kwa roho moja kuwa brother wewe hujui mimi nimetoka wapi na nakwenda wapi hivyo huwezi kujua hata hili litakujaje kwangu,” aliongeza.

Rich Mavoko amekuwa juu tangu alipojiunga na lebo hiyo ya WCB na kuachia wimbo wake ‘Ibaki Story’ unaozidi kufanya vizuri kwenye TV na Radio.

Drake Avunja Rekodi Ya 50 Cent Kwenye Chati Za Billboard Top 100


drake

Drake aweka rekodi mpya kwenye Billboard Top 100 baada ya wimbo wake wa ‘One Dance’ aliomshirikisha Wizkid kukaa kwa wiki sita kwenye chati hizo.
drake
Wimbo huo wa Drake umevunja rekodi iliyokuwa inashikiliwa na 50 Cent kwa wimbo wake wa ‘Candy Shop’ kukaa kwa wiki sita kwenye chati hizo, lakini pia albamu ya ‘Views’ nayo imeendelea kuweka rekodi kwenye chati hizo tangu alipoiachia April 28 mwaka huu.
Kwa upande wa wasanii wa kike Adele bado anaongoza kwenye chati hizo za Billboard Top 100 kwa wimbo wake wa ‘Hello’kukaa wiki sita.

Watch New Video | Shetta ft Dully Sykes & Tunda Man Mdananda | Official Video


Watch & Download New Video | Young Killer Ft. Mr Blue - Kumekucha

Watch New Video | Wakili - Sikuhukumu (Official Video)

Picha: Baraka Da Prince Akimdhalilisha Linah Ukumbini, Anaswa Akishika Kifua cha Linah

Baraka na Linah waliokuwa miongoni mwa mastaa waliokuwa kwenye ratiba ya kuburudisha siku hiyo, walifanya tukio hilo walipokuwa nyuma ya jukwaa (back stage) walipokuwa wakisubiri muda wao wa kutumbuiza ufike.

Paparazi wetu aliyekuwa akifanya ziara ya kushtukiza mara kwa mara back stage, kuna wakati alifanikiwa kumkuta Baraka akiwa ameingiza mkono kwenye kifua cha Linah huku mrembo huyo akionekana kumpa ushirikiano.

“Mh! Huu ni udhalilishaji, hata kama wameamua kuwa na uhusiano, kwa nini haya mambo wasifanyie chumbani? Baraka anamdhalilisha tu Linah. Naye sijui kwa nini anakubali kuingizwa mkono vile,” alisikika shuhuda mmoja.

Alipoulizwa na paparazi wetu kuhusiana na tukio hilo na kama ana uhusiano wa kimapenzi na Baraka, Linah alidai haoni tatizo kwani atakuwa amerejea kwenye himaya yake ya zamani.

“Naona ni bora kumrudia wa zamani ambaye nimemzoea,” alijibu Linah na kuomba aachwe.

Kwa upande wake Baraka ambaye inafahamika ni mpenzi halali wa mtoto mzuri Naj, hakutaka kuzungumzia chochote kuhusiana na tukio hilo zaidi ya kuishia kucheka tu.

Linah na Baraka waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi kabla ya kila mmoja kuchukua hamsini zake hadi waliponaswa wikiendi iliyopita ufukweni hapo.
 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes