BREAKING NEWS

Wednesday 15 June 2016

Master J na Shaa kufunga ndoa

Mtayarishaji mkongwe wa muziki nchini, Joachim Kimaryo ‘Master Jay’, ameweka wazi mpango wake wa kufunga ndoa na mpenzi wake wa muda mrefu, Sara Kaisi ‘Shaa’.
Shaa na Master Jay
Master J amesema Shaa atakuwa mke bora kwake kwani tayari ameshaishi naye kwa miaka 10 bila matatizo yoyote.
“Miaka 10 niliyoishi naye nimemwelewa vizuri, anastahili kabisa kuitwa mke wa Master J hapa nafanya taratibu za kumuoa ili tuishi maisha ya mke na mume,” Master J aliliambia gazeti la Mtanzania.
Mtayarishaji huyo wa muziki alisema kwamba anampenda Shaa kwa sababu ni msichana anayejielewa, licha ya kuwa msanii hasahau jamii inayomzunguka huku akijituma sana katika kazi zake zote kwa ujumla

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © 2014 Kali Za Wana. Designed by OddThemes