Hutakiwi kushangaa siku ukisikia lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond kuwa ipo juu zaidi ya Mavin Records inayomilikiwa na Don Jazzy, hiyo ni kutokada na mikakati pamoja na jitihada zinazozidi kuwekwa na uongozi wa lebo hiyo.
Mpaka sasa lebo ya WCB inawamiliki wasanii wanne akiwemo Diamond, Harmonize, Raymond na Q Boy Msafi huku kukiwa na taarifa za chini chini kuwa tayari Rich Mavoko ameshamwaga wino wa kuwa chini ya lebo hiyo huku bajeti yake ikiwa tayari imeshawekwa pembeni na tayari amesharekodi wimbo pamoja na video iliyofanyika huko Afrika Kusini. Lakini pia nje ya kutafuta vipaji kwenye hili analolifanya Diamond ni biashara kubwa ambayo itafanya akaunti zake za benki kujaa kila siku.
Hiki ndicho kitaweza kuipaisha lebo ya WCB kuwa kubwa zaidi.
Ukubwa wa jina la Diamond
Hili halina ubishi kwa sasa Diamond amekuwa ni miongoni mwa wasanii wenye majina makubwa kwenye tasnia ya muziki kwa Afrika kwa sasa. Hicho ni kitu ambacho kimemfanya kujitengenezea fan base kubwa kutokana na kazi zake anazofanya, lakini pia ana uwezo wa kuwatengenezea connection wasanii wa lebo yake [WCB] kufanya kazi na msanii yeyote wa Afrika endapo muda utaruhusu kutokana na jina lake huku yeye mwenyewe akizidi kujitafutia connection za Marekani na Ulaya kama walivyoanza kwa Harmonize kufanya kazi na Korede Bello kutoka Mavin Records lakini pia Harmonize aliwahi kusema ana kazi na Kiss Daniel wa Nigeria.
Mashabiki wanaomsupport Diamond
Diamond ni msanii mwenye washabiki wengi wanaomsupport ambao wapo tayari kupambana na lolote endapo wataona msanii wao anaandamwa na na maneno kutoka upande mwingine. Kutokana na hilo uongozi wa WCB unaweza kutumia pointi hiyo kuifanya lebo yao kuwa juu zaidi kama wanavyofanya sasa kwa Harmonize na Raymond kutembelea nyota ya Dangote.
Menejimenti ya WCB
Uongozi wa WCB ukiongozwa na Salaam pamoja na Babu Tale umefanikiwa kufaulu kwenye suala la mipango na kujiamini kwenye kila wanalolifanya na hawashindwi kujaribu. Kutokana na uwezo wao walionao wanaweza wakaifanya lebo ya WCB kufika mbali zaidi lakini itachukua muda mpaka kufika huko.
Source:Bongo5
Monday, 30 May 2016
Yasome Hapa : Mambo Matatu yanayoipa Nguvu Lebo ya Wasafi Kufika Mbali
Posted by Mkali Town on 05:12 in Entertainment | Comments : 0
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment