Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo.
Tayari nimezikusanya stori za Magazeti ya May 21 2016 na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine, moja ya stori kubwa ni hii kauli ya mtaalamu wa lishe wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Denis Mbinga katika mahojiano na Gazeti la Mtanzania.
Katika mahojiano hayo Mbinga alisema matatizo ya watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa , mgongo wazi na magonjwa mengineyo katika siku za karibuni yameongezeka kutokana na ulaji wa vyakula visivyofaa na hasa chipsi na vile vilivyosindikwa viwandani.
Chipsi hatari kwa wajawazito, husababisha watoto kuzaliwa na vichwa vikubwa na mgongo wazi pic.twitter.com/cokU8aBoIC
— Goodluck Mathias™ (@gudmathias) May 21, 2016
Post a Comment